The House of Favourite Newspapers

Mbuta Nanga Awapa Somo Mastaa Wanaotumia Bidhaa Feki, Awapa Ujanja

0
Mbuta Nanga akifungua shampeni kuashiria uzinduzi huo.

 

Staa wa Bongo Muvi na Mfanyabiashara maarufu Bongo na nchini Uingereza Frollah Lyimo a.k.a Mbuta Nanga amewapa somo mastaa wanaotumia bidhaa feki ikiwemo vipodozi au mkorogo na mavazi kuacha kutumia bidhaa hizo zisizo na ubora na kutumia bidhaa orijino ambazo kwa sasa zinapatikana kwenye duka lake liliolopo Kinondoni Manyanya Dar ngambo na American Chipsi.

Sehemu ya wageni waalikwa kwenye uzinduzi huo.

 

 

Mbuta Nanga alisema hayo wakati akizindua duka lake hilo jipya liitwalo Mbuta Nanga Mix ambapo aliwaambia mastaa na wananchi wengine waache kutumia bidhaa feki na kufika dukani kwake hapo kupata bidhaa OG kutoka nchini Uingereza na nchi nyingine zinazotengeneza bidhaa OG.

Mbuta Nanga na Mumewe wakifurahia pamoja na wageni waalikwa waliohudhuria hafla ya uzinduzi huo.

 

 

Mbuta Nanga aliyekuwa na mumewe kwenye uzinduzi wa duka hilo alisema anamshukuru sana mumewe huyo aliyemtaja kwa jina la Ngwesa na kuongeza kuwa jamaa huyo ndiyo kila kitu kwenye maisha yake.

Mbuta Nanga na mumewe wakifurahia.

 

 

Amesema Ngwesa ndiye aliyempa wazo la kuwezkeza duka hilo hapa nchini na kuacha kuwekeza Uingereza peke yake. “Siyo kila kilicho bora kiuziwe Ulaya vingine tunatakiwa kuvileta hapa nchini na kuwauzia Watanzania ambao nao wanastaili kupata bidhaa bora”, alisema Mbuta Nanga.

Akionesha moja ya bidhaa inayopatikana kwenye duka hilo.

 

 

Baada ya kusema hayo Mbuta Nanga na mumewe wakiwa na mabaunsa walikata utepe kuashiria uzindizi wa duka hilo la kisasa.  HABARI/PICHA NA RICHARD BUKOS /GPL   

Leave A Reply