The House of Favourite Newspapers

MC Balaa Atikisa Shangwe za Eid, Dar Live

0
MC Balaa akifanya balaa stejini.

MKALI wa Singeli, Mc Balaa ambaye anatamba na ngoma ya Nakuja usiku wa kuamkia leo alifanya bonge la balaa ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem, Dar ambapo kulikuwa na shamrashamra za Eid El Fitri.

Warembo wakinyonga baada ya kupagawishwa na swaga za Mc Balaa.

Mc Balaa alifanya balaa hilo baada ya kuachiwa steji na mwanadada Zuchu kutoka familia ya WCB ambaye naye alipiga shoo iliyoacha gumzo kwenye jukwaa hilo.

Nikienda huku masela mtakuja? Nikirudi huku masela mtakuja? Ndivyo MC Balaa alivyokuwa akiwapelekesha masela.

Ngoma hiyo ya Nakuja ambayo ni kama kisa hicho kimeshawakuta wengi mashabiki waliofurika ukumbini hapo walisikika wakiimba sambamba baadhi ya mashairi yake haswa pale “Mbona hutokei mamiloo, Nimechoka kusubiri mamiloo, Kama hutokei niambie”.

Jamaa alikuwa ndiye aliyehitimisha shoo ya ndani ya kiwanja hicho na kuwaacha mashabiki wakiwa wameridhishwa na burudani ya aina yake.

HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS /GPL

Leave A Reply