The House of Favourite Newspapers

Tanasha: Diamond Hakujali Penzi Letu

0

TANASHA Donna ambaye ni mzazi mwenza wa msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, ametoa kauli nzito iliyoibua mshangao kwa wafuasi wake.

 

Tanasha ambaye ni msanii wa muziki wa Kizazi Kipya wa nchini Kenya anasema kuwa, alitarajia kuolewa miaka miwili iliyopita, lakini mwanaume aliyekuwa naye ambaye ni Diamond au Mondi hakujali na kuliheshimu penzi lao.

 

Tanasha aliyasema hayo wakati akimuandikia waraka mzito mumewe mtarajiwa ambaye hakumtaja jina.Hata hivyo, katika maelezo yake hayo ndipo akajikuta akitoboa siri iliyomfanya aachane na Mondi; siri ambayo hakuwahi kuitoa.

Aliandika; “Mpenzi mume wangu mtarajiwa wa mwaka 2023…tunaweza kujenga maisha yetu ya baadaye pamoja.

 

“Lakini weka akilini mwako kwamba sichezi mchezo, ama uwe wangu au usiwe kabisa wa kwangu.“Kama ukiona msichana akikuzengea ni bora umuambie kwaheri au mimi ndiye nitakuambia kwaheri.

 

“Kama msichana akikutumia emoji ya moyo na macho, ni bora ukamjibu kwa emoji za amani au kumzuia kabisa.“Kama mwanamke akikuambia anakutamani, ni bora ukamwambia mchumba wako anakutamani pia, kama hutafanya hivyo, basi mimi nitakutakia kila la heri, usicheze michezo hiyo, heshimu uhusiano wako wa kimapenzi na ninakuahidi, tutakuwa salama.

 

Kimsingi Tanasha alitaka kusema kwa kifupi kuwa, sababu iliyomfanya kuachana na aliyekuwa mumewe mtarajiwa, Mondi ilikuwa ni kwamba jamaa huyo hakuheshimu uhusiano wao wa kimapenzi na badala yake alikuwa akirukaruka na wanawake wengine.

 

Staa huyo mwenye rekodi zake kwenye muziki nchini Kenya hakuthibitisha habari hizo kama kweli hiyo ndiyo sababu iliyomfanya kutengana na baba wa mtoto wake kuwa hakuheshimu mapenzi yao.

Kama ambavyo wengi wanajua, Zarina Hassan ‘Zari’ ambaye ni mzazi mwenza mwingine wa jamaa huyo, alitengana na Mondi kwa sababu hizohizo alizozitoa Tanasha kuwa, alimkosea heshima kupitia mpenzi wake mwingine wa zamani, Wema Sepetu.

Stori; Mwandishi Wetu, Dar

Leave A Reply