The House of Favourite Newspapers

MC Pilipili ampa shavu Barnaba

0

Mc-PilipiliMC Pilipili.

MKALI wa vichekesho vya majukwaani Bongo anayefahamika zaidi kwa jina la MC Pilipili, hivi karibuni amempa shavu mwanamuziki anayekimbiza kwenye gemu la Bongo Fleva, Barnaba ambaye watakuwa naye kwenye tamasha lake litakalofanyika jijini Mbeya ambalo linajulikana kwa jina la Cheka Vicheko vya Juu Nyanda za Juu.

barnaba1Barnaba

Akizungumza na mtandao wetu, MC Pilipili alisema, ameamua kumpa shavu hilo Barnaba kwa sababu ni mtu anayefahamu vizuri juu ya uwezo wake na anauhakika atamsaidia sana katika tamasha hilo litakalofanyika Juni 3, mwaka huu katika Ukumbi wa Tugimbe Mafiati ambapo atapiga shoo ambayo haijawahi kutokea.

“Barnaba ni mwanamuziki mzuri na ninapenda kufanya naye kazi, watu wa Mbeya wategemee kupata vitu adimu kutoka kwa mwanamuziki huyo lakini zaidi mimi maana nimejiandaa kuwavunja mbavu kwelikweli,” alisema MC Pilipili.

Leave A Reply