The House of Favourite Newspapers

MC Pilipili Hawezi Kuzuia Machozi

0

KOMEDIANI na mshehereshaji maarufu Bongo, Emmanuel Mathias ‘MC Pilipili’ amefunguka kuwa, katika maisha yake, hawezi kujikaza kama mwanaume ndiyo maana machozi yanamtoka kila linapokuja suala la furaha au huzuni.

 

Akichezesha taya na Amani, MC Pilipili amesema anawashangaa watu wanavyoona ajabu yeye kulia, laki ni ukweli ni kwamba ndiyo hisia zake zinavyomtuma.

 

“Mtu ukionesha hisia zako, watu wanakusema na kukushangaa, siwezi kuficha hisia zangu hata siku moja, iwe wakati wa furaha au huzuni. hivyo nawaomba wajue na waniache ndivyo nilivyo,” amesema MC Pilipili ambaye aliangua kilio siku ya kumvisha pete ya uchumba mkewe, Qute Mena.

 

Mc Pilipili alifikia hatua ya kufunguka hayo kutokana na hivi karibuni kipande cha video yake akiangua kilio wakati akihojiwa na runinga moja Bongo kiliposambaa mitandaoni na watu kubaki wakimshangaa inakuwaje mwanaume analia kama mwanamke.

Stori: Imelda Mtema, Dar

Leave A Reply