The House of Favourite Newspapers

Mshtuko Dar! Vijana Wachinja, Wala Nyama Mbichi ya Paka

0

HUU ni zaidi ya mshtuko! Wakati watu wakiwa wamezoea kula nyama ya ng’ombe, mbuzi na wanyama wengine waliozoeleka tena ambayo imepikwa, mambo yamekuwa tofauti kwa vijana; Stanslaus Luchano ‘Ghost’ (23) na Nicholas Michael ‘Chaupepo’ (28) ambao Amani limewashuhudia wakichinja paka na kula nyama yake mbichi.

 

Awali, Amani lilipewa taarifa juu ya vijana hao kutumia nyama mbalimbali mbichi ya mizoga ya mbwa, kenge, minyoo, kaa, panya kunguru na viumbe wengine wote isipokuwa sumu ndipo lilipowatembelea nyumbani kwao Kimara- Suka, jijini Dar ili kufanya nao mahojiano.

 

Baada ya kufika nyumbani hapo wanapoishi, vijana hao walianza kuonesha aina ya maisha yao hayo kwa kumchinja paka, kumkatakata vipande vidogovidogo na kisha kula na ugali.

 

Kama hiyo haitoshi, walikula paka, kaa na minyoo ambayo walikuwa wameiandaa kwa siku hiyo.

Baada ya kushuhudia maajabu hayo, Amani lilizungumza nao mmoja baada ya mwingine kwa kuanza na Ghost:

 

Amani: Hebu tupe kwanza historia yako kwa ufupi?

Ghost: Mimi tangu nikiwa mdogo nimelelewa na bibi yangu baada ya mama yangu kufariki dunia na baba yangu kunitelekeza, wakati nakua nikawa namuona bibi anakula ngedere wale wanaokula mahindi na vitu vingine vingi vya ajabuajabu lakini akivipika.

 

Kuna kipindi nilikuwa naogopa lakini baadaye nikaja kuzoea ile hali. Ilifika wakati nikawa naenda mtoni na mimi kuvua samaki ambao kuna muda nikawa nawakuta wamekaa pamoja na vyura, nikawa nakula tu vibichi.

 

Nakumbuka wakati nipo darasa la tatu kuna siku nilichukua yai nikalipasua halafu ndani nikakuta mtoto wa kuku nikamla vizuri tu na sikuzurika na chochote, hivyo hiyo ikanipa moyo wa mimi kuendelea kuvitumia vitu hivyo kwa kasi kiasi kwamba baada ya kuja huku mjini nikaanza kupata shida kwa sababu vyakula hivyo ni adimu.

 

Amani: Dar es Salaam ulifika vipi na ulikuja kufanya nini?

Ghost: Mimi ni mkulima mwaka 2014 kuna mtu alikuwa anahitaji mtu wa kumlimia shamba na bustani lake ambapo niliambiwa, nikakubali basi nikatumiwa nauli na mwisho wa siku ndiyo nikaingia hapa Dar.

 

Amani: Mara ya kwanza unaanza kuishi na watu wengine tofauti haukupata shida wakati wa kula?

Ghost: Nilichokuwa nakifanya ikifika jioni naondoka naenda mtaani kutafuta chakula kama paka, kenge, mbwa, minyoo nk kisha nakula hukohuko kwa sababu nilikuwa sitaki wajue na ukizingatia wale ni watu wa dini hivyo nikawa naogopa watanichukulia tofauti.

 

Amani: Huwa unakula chakula cha kawaida kwa siku mara ngapi?

Ghost: Kiukweli nisiwe muongo mimi chakula cha kawaida sili na hata nikijilazimisha kula naumwa.

Amani: Mara ya mwisho kula ilikuwa lini?

 

Ghost: Wiki kadhaa zilizopita niliingia kwenye mgahawa flani hivi nikala wali maharage na nyama ya ng’ombe baada ya muda tumbo lilianza kuniuma sana mpaka nikaenda kulazwa kwenye hospitali moja ipo Suka inaitwa Wema.

 

Nililazwa pale siku tatu na kutundikiwa dripu sita za maji, sasa siku ya nne ikabidi nimuite huyu rafiki yangu (Chaupepo) nikamwambia kwa siri kuwa anifuatie nyama mbichi buchani aniletee. Kweli alifanya hivyo akaenda kunichukulia akaniletea nikala, huwezi amini baada ya kula tu nikaanza kujisikia vizuri nikaruhusiwa kurudi nyumbani.

 

Amani: Vipi kuhusu majirani wanakuchukuliaje?

Ghost: Asilimia kubwa watu wanaotuzunguka wanatuogopa sana kwa sababu kuna muda mtu hawezi hata kukusalimia kwa mkono wala kukukaribisha chakula anachokula yeye.

Amani: Baada ya kuingia Dar sasa ni jambo gani ambalo ulilifanya na likafanya watu wakujue zaidi?

 

Ghost: Ilikuwa kuna barabara inatengenezwa ambapo kulikuwa na mitimiti sasa wakati katapila linatengeneza, kuna mti ukakatika na kuangusha kunguru aliyekuwa juu ya huo mti. Nikamchemsha na kumla. Tangu siku hiyo wakaanza kunifahamu.

Amani: Unajisikiaje baada ya kuona umetengwa na baadhi ya watu?

 

Ghost: Najisikia kawaida tu kwa sababu hiki ninachiokifanya ndio kinachoniweka mjini kwa watu kuniita kwenye matamasha yao.

Amani: Ikitokea umekosa hivi vitu huwa unakula nini?

Ghost: Nikikosa huwa naenda kwenye zile meza wanazokata matikiti kisha naokota yale maganda yake nakula au mboga za majani mbichi.

 

Amani: Hutumii uchawi wala mazingaombwe yeyote?

Ghost: Hapana situmii uchawi wala mazingaombwe haya ni kweli ndiyo maisha yangu.

Amani: Unategemea kuendelea kula hivi vitu mpaka lini?

Ghost: Huwezi kumzuia mtu kula chakula, siwezi kuacha hiki ndio chakula changu mpaka Mungu atakaponichukua.

 

Kwa upande wake Chaupepo, naye alisimulia jinsi alivyokutana na Ghost.

“Mimi ni dereva bodaboda, nilikutana na Ghost, akanipa wazo hili la kuwa tunakula vitu vya ajabu, awali nilikuwa mzito kidogo lakini baadaye niliridhia.

“Nilikubali sababu niliona tunaweza kujiongezea pia kipato kutokana na kuitwa na watu mbalimbali katika matamasha yao,” alisema.

 

Aidha, mke wa Chaupepo, Pendo alizungumza na Amani na kusema awali ilikuwa vigumu kumuelewa lakini baadaye akakubaliana naye baada ya kuona hapati madhara yoyote pindi anapokula nyama hizo mbichi.

“Nilimuelewa kwa sababu pia nampenda na sasa tuna miaka miwili ya ndoa, maisha ni mazuri. Mimi napika tu ugali, mboga yake mbichi anaitengeneza mwenyewe,” alisema Pendo huku akibainisha kuwa yeye na mtoto wao mmoja wanakula mboga za kawaida.

Ili kuyapata mahojiano kamili, ingia You Tube, tafuta Global TV.

Stori: Memorise Richard, Amani

Leave A Reply