The House of Favourite Newspapers

MC Pilipili kuwavunja mbavu Mbeya leo

0

Mc-PilipiliMKALI wa vichekesho vya jukwaani, Emmanuel Mathias ‘MC Pilipili’ kwa mara ya kwanza leo (Juni 3) anatarajiwa kuibukia Mbeya na kuwavunja mbavu wakazi wa mkoa huo ndani ya Ukumbi wa Tugimbe Mafiati.

Akizungumza na Showbiz, MC Pilipili ambaye ni mkali wa vichekesho vya jukwaani alisema, shoo yake hiyo itakwenda kwa jina la Cheka Vicheko vya Juu Nyanda za Juu na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla.

“Natarajia kuandika historia kwa mara ya kwanza jijini Mbeya, sidhani kama kuna msanii wa vichekesho vya jukwaani aliyewahi kuweka rekodi ya kuchekesha, tukutane (leo) pale Tugimbe,” alisema MC Pilipili. Shoo hiyo itasindikizwa na mkali wa Bongo Fleva, Elius Barnaba.

Leave A Reply