The House of Favourite Newspapers

Wasomaji Wamelikubali Toleo Jipya Gazeti la Ijumaa

0

1.    Wasomaji wa Gazeti la Ijumaa toleo jipya wakiwa katika picha ya pamoja na Maofisa wa Global, Yohana Mkanda na Jimmy Haroub (wenye kofia nyekundu) katika stendi ya daladala maarufu ya mawasiliano, maarufu Simu 2000.

2Wasomaji wa Ijumaa wakijaza kuponi za Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba ili kushiriki droo kubwa ya shinda nyumba itakayofanyika mwezi huu.

3Msomaji wa Gazeti la Ijumaa (katikati) akielekezwa kujaza kuponi yake na Ofisa Masoko wa Global, Yohana Mkanda.

4Wasomaji wa toleo jipya la Gazeti la Ijumaa wa eneo la stendi ya daladala ya Kawe wakilisoma gazeti hilo sambamaba na Ofisa Masoko, Yohana Mkanda (mwenye fulana nyeupe).

5Msomaji wa Gazeti la Ijumaa (kushoto) akijaza kuponi yake ili kushiriki Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba.

GAZETI la Burudani linalotoka kila siku ya Ijumaa ambalo limekuja na sura mpya na bei mpya ya shilingi 1,000, leo baadhi ya wakazi wa jiji la Dar walionekana kulipokea kwa shangwe baada ya kukutwa wakilisoma huku wengine wakijaza kuponi za kushiriki Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba.

Maofisa Masoko wa Global Publishers,Yohana Mkanda na Jimmy Haroub walitembelea maeneo mbalimbali ya jiji na kukuta wasomaji wa gazeti hilo la Ijumaa wakilisoma na kujaza kuponi za kushiriki Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba.

Akizungumza juu ya maboresho hayo Mhariri wa gazeti hilo, Amran Kaima alisema:

“Wasomaji wa habari za burudani nawaombeeni mzidi kulisoma Gazeti la Ijumaa ambalo tumeliboresha zaidi na kuwa na mwonekano mzuri, hivyo niwahakikishieni tutazidi kuliboresha na kupata maoni mbalimbali kutoka kwenu wasomaji ambayo tutayafanyia kazi,”alisema Kaima.

NA DENIS MTIMA/GPL.

Leave A Reply