The House of Favourite Newspapers

Mchekeshaji Idris Alamba Shavu la Ubalozi

Idris Sultan akionesha cheti cha ubalozi alichopewa.

DAR ES SALAAM: Msanii mchekeshaji, Idris Sultan leo, Februari 1, 2017 ameteuliwa kuwa Balozi wa Global Peace Foundation, nchini Tanzania pia atawakilisha katika matawi 25 ya mikutano mbalimbali duniani.

Mkurugenzi wa Global Peace Foundation, Martha Nghambi akizungumza na wanahabari wakati wa kumtambulisha Idris.

Mkurugenzi wa Global Peace Foundation, Martha Nghambi amesema wamemteua  Idris kwa sababu tayari ana sifa za kutuwakilisha Watanzania, hivyo anaweza ni kijana ambaye anaweza kuwafikia watu wengi zaidi.

Martha Nghambiakimkabidhi Idris cheti cha Ubalozi.

Naye Idris amesema kuwa amepokea kwa shangwe kuteuliwa kuwa balozi wa amani nchini na kuwakilisha vijana wa Kitanzania katika mikutano mbalimbali itakayofanyika duniani.

Idris Sultan akizungumzana wanahabari.

“Amani ina mambo mengi sana, kuwa na upinzani wa kupitiliza huo ni uvunjifu wa amani, kuwa na timu za kuwafagilia wasanii kupitiliza ni uvunjifu wa amani hata baba anayemlazimisha mtoto wake asome udaktari wakati yeye anapenda kuwa mwalimu ni uvunjifu wa amani. Unadhani huyo mtu atakuwa Daktari mzuri kama siyo kufanya sivyo ndivyo,” alisema Idris.

Cheti cha Ubalozi alichopewa Idris.

Na:Gabriel Ng’osha/GPL

Comments are closed.