The House of Favourite Newspapers

Jike Shupa Atetea Ushosti na Wema

Zena Abdallah ‘Jike Shupa’

WAKATI baadhi ya watu wakiusengenya urafiki wa ghafla ulioibuka baina ya Zena Abdallah ‘Jike Shupa’ na Wema Sepetu, muuza sura huyo kwenye video ameibuka na kuutetea ushosti huo, akiwataka watu kuwaacha, kwani kwa muda mrefu, amekuwa akimpenda muigizaji huyo maarufu kama Madam.

Siku chache zilizopita, katika mtandao wa kijamii wa Instagram, kuliwekwa kipande cha video kikimuonyesha Wema akijiita ‘Wema Shupa’ hali iliyowafanya mashabiki kumuona Miss Tanzania huyo wa mwaka 2006 kama amepotea njia kuwa na urafiki na mwanamke huyo anayefanana sura na Shilole.

Lakini Jike Shupa akizoza na Za Motomoto News, alisema; “Kiukweli tangu zamani nampenda sana Wema, watu wanazungumza mengi, eti Wema kwangu amepotea, sitishiki wala siumizwi, siwahofii wao, mimi nampenda Wema na nitaendelea kumpenda maana nimetokea kumkubali sana,” alisema Jike Shupa.

Comments are closed.