The House of Favourite Newspapers

MCHIMBA VISIMA, MKULIMA WALAMBA MILL 85 ZA PREMIER BET

Washindi wa Jackpot ya Kampuni ya Bahati Nasibu ya Premier Bet Tanzania, Flavian Msigala mkazi wa Mtongani, Kunduchi jijini Dar es Salaam mtaalam wa visima (wa pili kutoka kulia) na Robert Daniel mkazi wa Mpanda ambaye ni mkulima (wa pili kutoka kushoto) wakati wakikabidhiwa zawadi zao na Premier Bet hivi karibuni.
Kampuni ya Bahati Nasibu ya Premier Bet Tanzania hivi karibuni imekabidhi hundi ya shilling million 85 kwa washindi wawili wa Jackpot ya soka kwa Flavian Msigala kutoka Dar es Salaam na Robert Daniel kutoka Mpanda ambapo kila mmoja atajinyakulia mill 42.5.

Akizungumza na waandishi wa jijini Dar es Salaam, Afisa rasilimali watu na Meneja utawala Amanda Reuben Kombe amesema kuwa kampuni hiyo pamoja na Michezo mingine wamekua wakiendesha mchezo wa Jackpot ya soka kupitia vituo vya mawakala wao na maduka kote nchini Tanzania.

 

Aidha alisema ikampuni hiyo, imekua ikiendesha shughuli zake kwa kufuata misingi yote ya kubashiri timu ambayo imewekwa, hivyo amewataka wananchi kuendelea kubashiri michezo mbalimbali kupitia Premier Bet ili kuboresha maisha yao endapo wataibuka washindi na kuachana na propaganda kuwa washindi hupangwa.

“Kampuni yetu ya Premier Bet huendeshwa kwa kufuata kanuni na sheria ya michezo ya kubahatisha hivyo nawaomba watanzania waendelee kubashiri michezo mbalimbali hasa kwenye Jackpot na kutuamini ili tuweze kubadilisha maisha yao,” alisema Amanda.
Kwa upande wake, mshindi wa jackpot hiyo kutoka Mpanda, Robert Daniel ameipongeza kampuni hiyo kwa kutenda haki ya kuweza kuwapatia fedha hizo ambazo zitawasidia kuendesha maisha yao.
“Naipongeza sana kampuni hii, kwani imeweza kubadilisha maisha yake, kutoka mkulima wa mpunga na mfugaji ambapo kwa anaweza kumiliki nyumba na kuwa mfanyabiashara na kuweza kuendesha maisha yake kwa uhakika ” alisema Robert.

Comments are closed.