The House of Favourite Newspapers

Tetemeko la Ardhi Laitikisa Mbeya na Rukwa

TETEMEKO  la ardhi lililodumu kwa takriban dakika moja leo mchana, Alhamisi Machi 21, 2019, limetokea mkoani Mbeya na kuzua taharuki huku baadhi ya wananchi na wafanyakazi katika ofisi mbalimbali wakitimua mbio.

Baadhi walilazimika kuacha ofisi zao huku waliopo majumbani wakitoka nje ya nyumba zao.

 

Mwandishi wetu alishuhudia Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya,  James Kasusura,  na Meya wa jiji hilo,  David Mwashilindi,  na wafanyakazi wengine wa ofisi zilizopo Uhindini jijini hapa, wakitimua mbio.

 

“Kumbe na wewe unajua kukimbia,” alisikika akitamka Kasusura akimtania Mwashilindi na kuongeza:

“Tulikuwa na maongezi na meya wangu lakini nikashangaa viti vinasogea ikanibidi nichukue hatua kukimbia ila cha kushangaza wakati natoka sijamuona meya katoka kupitia njia gani.”

Watumishi wa kampuni na mashirika ya umma yenye ofisi zake jijini hapa walionekana kukaa vikundi na kuzungumza kuhusu tetemeko hilo.

Comments are closed.