The House of Favourite Newspapers

Mchizi Mox Apambana na Hali Yake

0

MKALI wa kitambo kunako Bongo Hip Hop, Taikuni Ally ‘Mchizi Mox’ amesema, yupo fiti na anapambana na hali yake ili kurudi kwenye gemu na ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la Fala.

 

Mox ambaye amewahi kutisha na ngoma kibao kama Mambo Vipi, Nipende Nichukie na nyinginezo ameiambia OVER ZE WEEKEND kuwa, ukimya wake una mshindo mkubwa.

 

“Nilikuwa kimya, lakini kama wasemavyo wahenga, kimya kingi kina mshindo mkubwa ndivyo itakavyokuwa baada ya kuanza upya kuachia ngoma zangu, nimeanza na Fala ambayo maandalizi yote ya Audio na video yamekamilika,” amesema Mox.

STORI: RICHARD BUKOS, DAR

 

Leave A Reply