The House of Favourite Newspapers

Mchumba Jack Dustan ajitutumua na ka-Vitz

0

Jack (2)Jacqeuline Dustan kwenye gari aliyonunuliwa.

Imelda Mtema

BAADA ya kuhakikishiwa ndoa, mchumba wa mrembo aliyejipatia jina kupitia Shindano la Maisha Plus Season 11, Jacqeuline Dustan, Hamis Ally amejitutumua kwa kumnunulia mkewe mtarajiwa huyo kagari aina Toyota Vitz.

Jack (1)Wawili hao wanatarajia kufunga ndoa mwanzaoni mwa mwaka ujao na baada ya kila kitu kwenda sawa ikiwa ni pamoja na kulipiwa mahari, Hamis aliona atoe zawadi hiyo ili kumuonesha Jack kuwa amefurahi kuona ndoto zake za kuishi naye zinaelekea kutimia.

Akizungumza na Ijumaa mara baada ya kunaswa na gari hilo, Jack alisema: “Yaani hakuwa akiamini kwamba tutafi kia hatua hii na ndiyo maana amenipa hii zawadi ya gari. Ni gari f’lani niliyokuwa naipenda sana.”

Leave A Reply