MCHUNGAJI ALIYETABIRI MABADILIKO SERIKALI YA JPM 2019 – VIDEO

UNABII UMETIMIA! Hivyo ndivyo unavyoweza kusema ikiwa ni siku 8 tu tangu Mtumishi wa Mungu, Pastor Malachi Joseph kutabiri kuwa Rais Dkt. John Magufuli atafanya mabadiliko katika taasisi na baashi ya wizara Serikalini ya Tanzania kwa mwaka 2019.

 

Pastor Malachi alitoa utabiri huo katika ibaada maalum ya kuliombea Taifa la Tanzania iliyofanyika usiku wa Desemba 31, 2018, kwenye mkesha wa kuukaribisha mwaka mpya 2019, katika Kanisa la Christ Mandate h lililopo Kigogo, jijini Dar es Salaam mkabala na Kituo cha Polisi Kigogo na kusema kuwa maono hayo amepewa na Mungu huku akieleza kwamba kupanguliwa kwa viongozi hao kutaibua mshituko miongoni mwa wananchi.

 

“Mwaka 2019 kutakuwa na maendeleo kwa Taifa, lakini kutakuwa na mabadiliko kwa vyeo vya watu katika taasisi na mamlaka mbalimbali za Serikali, usishangae kuhusu hilo,” alisema Pastor Malachi.

 

Baada ya kutoa nabii hiyo, Pastor Malachi ambaye amekuwa maarufu kwa kutoa mapepo, kuharibu nguvu za giza zilizokufunga, magonjwa sugu kama kisukari na presha, aliwaongoza waumini wote katika hilo kuliombea Taifa na viongozi wake wote chini ya Rais Magufuli.

 

Siku nane tu baadaye, Jumanne, Januari 8, 2019, utabiri wa Pastor Malachi ulitimia baada ya Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi, aliitangaza mabadiliko madogo katika baraza la mawaziri na uteuzi wa viongozi wapya kadhaa uliofanywa na Rais Magufuli ambapo alimteua Dotto Biteko kuwa Waziri wa Madini huku aliyekuwa waziri wa Wizara hiyo, Angela Kairuki akimhamisha na kumteua kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu /Uwekezaji (Wizara mpya).

 

Wengine waliyoteuliwa na Rais ni makatibu wakuu wane; Katibu Mkuu (Tamisemi), Joseph Nyamhanga, Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Zainab Chaula na wengine huku Rais akiifuta nafasi ya Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na kumteua aliyekuwa Balozi wa Wizara ya Afya, Dr. Mpoki Ulisubisya kuwa balozi ambapo kituo chake kitatangazwa baadayee.

 

Aidha, Januari wakati Rais Magufuli akiwaapisha viongozi hao alisema ataendelea kufanya mabadiliko kila mahali, ambapo atakuwa hajajaridhika, anayehuika ataondoka, hata kama ni Biteko aliyemteua juzi huku akiwataka wote kuwajibika kwa maslahi ya Watanzania na kwa mujibu wa sheria.

 

KUTAZAMA VIDEO YA UTABIRI HUO, INGIA YOUTUBE CHANNEL YA PASTOR MALACHI J. MINISTRIES AU

BOFYA HAPA ===> MALACHI J. MINISTRIES

Loading...

Toa comment