The House of Favourite Newspapers

Mchungaji Ashambuliwa na Nyoka Akikemea Mapepo

0

HALI  ya kutatanisha imezuka Kasikeu, Makueni nchini Kenya wakati Pasta aliyeitwa kuwakemea mapepo aliposhambuliwa na nyoka katika nyumba ya jirani ya muumini wake.

 

Katika kisa hicho kilichochapishwa kwenye gazeti la Taifa Leo, mwenye nyumba hiyo alimwendea jirani yake kumuomba usaidizi akilalamika kuhusu kusumbuliwa na mapepo.

 

Jamaa huyo alimuahidi kumletea mchungaji aliyesifika katika kuwakemea mapepo na kuwafukuzilia mbali na kumuondolea taabu ya mizimu hao.

 

Pasta huyo aliyeitwa kuwakemea mapepo waliokuwa wakimsumbua bwana huyo kwenye boma lake hakusita kufika kwa kazi hiyo. Siku ya tukio hilo la kustaajabisha, mchungaji huyo alifika nyumbani humo tayari kwa kuwakemea mapepo hao.

 

Kabla kuanza maombi, alimwomba jamaa huyo kutoa sadaka ili kumpa Mungu haki yake na kufanikisha shughuli hiyo. Jamaa alitoa KSh 5,000 kisha pasta akaanza maombi huku akizunguka kila upande ya nyumba hiyo.

 

Alipofika nyuma ya nyumba hiyo, nyoka wawili walijitokeza ghafla na kuanza kumshambulia mchungaji huyo aliyetimka mbio kujinusuru huku akipiga nduru yaani kelele.

 

Baada ya pasta kukimbia, inadaiwa kuwa nyoka hao walitoweka kimuijiza na kuwaacha wau wengi vinywa wazi wengine wakikimbia kwa woga mwingi.

 

Mwenye nyumba hiyo alilazimika kujifungia ndani ya nyumba yake ishara ya kuogopa huku wenyeji wakidai kuwa yeye ndiye mmiliki wa majoka hao.

Leave A Reply