The House of Favourite Newspapers

MCHUNGAJI: WEMA AOKOKE ILI KUONDOA MIKOSI…

Daud Mashimo ‘Komando Mashimo’

WITO! Mchungaji wa Mitume na Maaskofu Tanzania wa Kanisa la Emmaus Bible Church Pentecostal lenye makao yake Mbezi-Luis jijini Dar, Daud Mashimo ‘Komando Mashimo’ amemtaka staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu aokoke ili kuondokana na mikosi.  Wema amekuwa akipata majanga mara kwa mara na wakati mwingine akijikuta kwenye vyombo vya sheria hivyo baadhi ya watu kuamini ana mikosi.

Jana Mchungaji Mashimo aliibuka kanisani kwake na kusema kuwa ili Wema aondokane na mikosi na kashfa mbalimbali zinazosababisha kufunguliwa kesi mara kwa mara, ni lazima aokoke kwani ana Mungu ndani yake. Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Mashimo alisema amekuwa akimuombea Wema mara kwa mara na kubezwa na watu, lakini anafanya hivyo kwa sababu alioteshwa kufanya hivyo kwa ajili ya kuhakikisha anamuokoa staa huyo ambaye Mungu anamhitaji.

“Unajua watu hawajui kuwa mimi kuna kitu nimekiona kwa Wema na ni muda mrefu sana, unadhani kwa nini ninamg’ang’ania? Hata yeye anajua kwani mimi huwa sikurupuki. Wema anatakiwa kumfuata Mungu na akifanya hayo atashangaa maisha yake yatakuwa mazuri kwani ana kitu ndani yake. Mchungaji huyo alipohojiwa sababu ya kumuombea Wema tu na si wasanii wengine wakati Wema mwenyewe amekuwa akimkana, alidai mwanadada huyo ana kitu ndani yake, anamhitaji Mungu na kwamba anajua kuwa Wema hajawahi kumkana.

“Unajua Wema anaujua ukweli na kama amenikana nilipata habari zote kuwa kuna mtu alimshawishi kunikana, lakini bado nasisitiza kuwa Wema atamfuata Mungu kwani maombi niliyofanya si ya kitoto juu yake na watu watashangaa siku moja,” alisema Mashimo. Alisema hataicha kazi ya kumuombea Wema mpaka atakapotimiza kile alichoambiwa na Mungu kwenye ndoto yake pale kitakapotimia.

Comments are closed.