The House of Favourite Newspapers

Mdada Apagawishwa Baada Kukabidhiwa Milioni 5 Ya Chawote

0
Meneja wa kanda ya kinondoni kutoka Tigo Beatrice Kinabo (kulia) na  Meneja  Mauzo wa Tigo  mkoa wa Mwananyamala Loid Kaaya (kushoto) wakimkabidhi mfano wa hundi Upendo Mkonya aliyejishindia Milioni 5 kupitia kampeni ya Chawote. 

Dar es Salaam 12 Julai 2023: Kampuni ya Tigo Tanzania imetoa kiasi cha shilingi milioni 5 kwa mshindi wa mwezi kwenye kampeni ya Chawote inayotolewa na kampuni hiyo.

Meneja wa kanda ya kinondoni kutoka Tigo Beatrice Kinabo amesema lengo la kampeni hiyo ni washiriki wengi zaidi kuvuna zawadi kutoka Tigo.

Naye Meneja  mauzo Tigo  mkoa wa Mwananyamala Loid Kaaya amesema watumiaji wa huduma za mtandao huo wataendelea kuvuna zawadi nyingi kama ilivyokuwa kwa mshindi huyo wa milioni tano Upendo Mkonya.

Kwa upande wake mshindi wa fedha hizo, Upendo Mkonya akionesha kupagawishwa na kitita hicho huku akiangua kicheko amesema atazitumia fedha hizo kujiendeleza zaidi kiuchumi na kuwasihi watanzania kuendelea kutumia huduma za Tigo ili kujishindia.

Tigo wamekuja na kampeni hiyo ya kuwazawadia watumiaji wa huduma mbalimbali za kampuni hiyo kampeni itakayodumu kwa siku 90.

Leave A Reply