The House of Favourite Newspapers

Mkuu wa Polisi nchini Kenya Apiga Marufuku Maandamano ya Upinzani

0

Mkuu wa polisi nchini Kenya amepiga marufuku wafuasi wa upinzani kuitisha maandamano haramu leo Jumatano kufuatia wimbi la hasira juu ya ongezeko la kodi iliyotangazwa na serikali ya Rais William Ruto.

Kiongozi wa upinzai Raila Odinga amewasihi Wakenya kuingia mitaani kupinga kupanda kwa gharama ya maisha, na watu watatu waliuawa kufuatia maandamano katika miji kadhaa siku ya Ijumaa.

Tume ya taifa ya haki za binadamu ya Kenya iliomba kufanyike uchunguzi wa kina kuhusu matukio yote yaliyoripotiwa ya ukatili wa polisi”, huku mashirika ya kutetea haki za binadamu ikiwemo Amnesty International yakilaani “watu kukamatwa kiholela.”

Inspekta jenerali wa polisi Japhet Koome amesema walioandaa maandamano hayo hawakuwapa polisi “taarifa zozote kuhusu maandamano yao yaliyopangwa wiki hii.

“Kutokana na hilo, maandamano hayataruhusiwa hivi leo. Njia zote za kisheria zitatumika kusambaratisha maandamano hayo,” alisema katika taarifa Jumanne jioni.

Siku ya Ijumaa, polisi walifyatua gesi ya kutoa machozi katika mji mkuu Nairobi, wakiulenga msafara wa Odinga, na walichukua hatua kama hizo dhidi ya maandamano katika miji ya Mombasa na Kisumu.

Muungano wa Odinga, Azimio, uliapa kufanya maandamano kila wiki dhidi ya sera za serikali ya Ruto.

#EXCLUSIVE: MSANII ANAYEDAI KUIBIWA WIMBO na ANJELLA AIBUA MAZITO, ALIVYOFOKEWA, AELEZA KWA UCHUNGU

Leave A Reply