The House of Favourite Newspapers

Mechi ya Simba, YANGA Yazijibu Tuhuma za Uchawi – Video

KLABU ya Soka ya Yanga imesema kuwa maneno ambayo yalikuwa yakiendelea katika mitandao ya kijamii ni kutokana na tukio la Jumapili kwenye mechi yao na Simba mshambnuliaji Ibrahim Ajibu alianzisha mpira kwa kuupiga nje jambo lilotafsiriwa na baadhi mashabiki wa Simba kuwa ni ushirikina.

 

Akijibu maswali ya wanahabri kwenye mkutano wake leo jijini Dar es Salaam, Msemaji wa yanga, Dismas Ten amesema alichokifanya Ajibu kwenye mechi hiyo siyo kigeni kwani hata wachezaji wa Timu za Ulaya huwa kina fanyika na si mara moja.

 

“Ni watu wachache sana wanaweza kuzungumzia ushirikina kwenye football, siyo kwamba Ajibu ndo kaanza kufanya hivyo, ipo timu ilishawahi kuingia kwa msitari mmoja hadi katikati ya uwanja, waache waamini wanavyoamini, huwezi kubadilisha mtu anahokiamini, hiyo ni saikolojia tu ya mpira kuwaweka watu sawa,” alisema Dismas.

 

Simba na Yanga walikutana Jumapili katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Saalam ikiwa ni muendelezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara na kutoa sare ya bila kufungana.

VIDEO: MSIKIE DISMAS TEN AKIFUNGUKA

Comments are closed.