The House of Favourite Newspapers

Mei Mosi Ilivyoadhimishwa Dar

0

Mgeni rasmi katika madhimisho hayo ya Mei Mosi 2017,  Margareth Sitta,  akizungumza katika sherehe hizo.

Mwenyekiti wa chama cha wafanyakazi Mkoa wa Dar es Salaam (Tucta), George Faustine,  akizungumza.

 

Magari ya makampuni mbalimbali yakipita mbele ya mgeni rasmi kuonyesha shughuli wanazozifanya wafanyakazi wake.

Wafanyakazi wa kampuni ya vinjwaji (pombe) wakipita mbele na gari lao kuonyesha bidhaa zao.

Gari la kuchimba visima na wafanyakazi wake wakipita mbele ya mgeni rasmi.    Baadhi ya wafanyakazi waliofika katika sherehe hizo.

 

WAKATI maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi kitaifa yakifanyika mkoani Kilimanjaro, jijini  Dar es Salaam wafanyakazi wameadhimisha sherehe hizo katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi alikuwa Mbunge wa Urambo, Mh. Margaret Sitta.

Katika sherehe hizo, makampuni mbalimbali ya serikali na taasisi binafsi zikiwemo hoteli, zimekuwa kivutio kikubwa baada ya kupita mbele ya mgeni rasmi na magari yao yakionyesha bidhaa wanazozalisha kutoka kwa  makampuni hayo au kuonyesha shughuli wanazozifanya hali iliyopelekea umati uliofika kwenye sherehe hizo kufurahia shughuli hiyo.

Akizungumza katika sherehe hizo, Mama Margareth Sitta amewataka wafanyakazi kujiunga katika vyama vya wafanyakazi ili  kupata haki zao za msingi ambazo wanaweza kuzikosa.

Kauli-mbiu ya mwaka huu ilikuwa “Uchumi wa viwanda uzingatie haki, maslahi na hesma ya wafanyakazi”.

Gari likiwa na bomba la maji baada ya kupita mbele ya mgeni rasmi.

Taswira ya Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam ulivyoonekana.

Meza kuu.

Na Denis Mtima| Global Publishers

 

Leave A Reply