The House of Favourite Newspapers

Membe: Mimi Ndiye Mgombea Urais wa ACT-Wazalendo

0

MGOMBEA urais kwa tiketi ya ACT-Wazalendo. Bernard Membe,  leo Septemba 22, 2020, kupitia ukurasa wake wa Twitter amekanusha taarifa  kuwa chama chake kimejiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katika ngazi ya kuwania urais.

 

Ameandika: “Mimi ndiyo Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha ACT – Wazalendo. Mimi ndiye niliyekabidhiwa Ilani ya Chama hicho kuinadi kote nchini kwenye Uchaguzi huu.  Taarifa zingine zinazosambaa kuwa tumejiunga na Chadema kwenye ngazi ya Urais siyo za kweli”.

 

Kauli yake inakuja baada ya Mwenyekiti wa ACT – Wazalendo Taifa, Maalim Seif Sharif Hamad kumuidhinisha Tundu Lissu (Chadema) kuwa mgombea wao wa urais wa Tanzania

Leave A Reply