The House of Favourite Newspapers

UVCCM Songwe Yamwandama Lissu Kila Kona

0

 

Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Mkoa wa Songwe umemtaka mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kuacha kufanya kampeni za chuki zinazolenga kuwagawa Watanzania.

 

Rai hiyo imetolewa Septemba 20, 2020 na Mwenyekiti wa UVCCM mkoani humo, Andrew Kadege wakati akizungumza na wananchi wa wilaya ya Momba ambako vijana wa CCM wamepiga kambi.

 

Kadege alimuonya Lissu kuacha kujaribu kuwagawa wananchi kwa aina ya kampeni anazofanya badala yake ajikite kwenye ilani ya chama chake.

“Lissu badala ya kunadi sera zilizomo kwenye ilani ya chama chake, anawagawa Watanzania kwa kuwajengea chuki dhidi ya Serikali ya awamu ya Tano ilihali akitambua mambo makubwa ambayo serikali hii imefanya.

 

“Tunamshauri afanye kampeni za kistaarabu, sisi wote ni Watanzania, asitugawe kwa chuki,” alisema Kadege.

 

 

Aidha, vijana hao wakiongozwa na mratibu wa kampeni za UVCCM Mkoa wa Songwe, Ombeni Nanyaro akiwa ameambatana Kadege wamepiga kambi katika wilaya ya Momba kusaka kura za mgombea urais, Dk. John Magufuli, wagombea ubunge na udiwani katika mkoa huo.

 

“Tunapita mtaa kwa mtaa huku tukinadi sera na kuielezea Ilani ya CCM kwa wananchi pia kumuombea mgombea wetu wa urais kura sambamba na wagombea ubunge na madiwani wote wa mkoani wa Songwe” alisema Nanyaro.

Leave A Reply