The House of Favourite Newspapers

Meneja: Anayemtaka Kakolanya Aje

Beno Kakolanya.

YUPO Huru! Ndivyo unavyoweza kusema kufuatia meneja anayemsimamia kipa Beno Kakolanya, Suleman Haroub kuweka wazi kuwa timu yoyote inayomhitaji mteja wake huyo iende kumsajili.

 

Beno Kakolanya ambaye aligoma kuendelea na Yanga tangu mzunguko wa kwanza wa ligi kwa sababu ya kudai baadhi ya haki zake za msingi ndani ya klabu hiyo ya Yanga.

 

Akizungumza na Championi Jumamosi, Haroub alisema kuwa, kwa sasa Kakolanya na Yanga wote wapo kwenye mchakato ya kuachana hivyo kama kuna timu zitahitaji huduma yake basi zipeleke ofa kwake kwa ajili ya mazungumzo.

“Kama kuna timu itamuhitaji Kakolanya walete ofa yao ili tuwasikilize kwani upande wa Yanga na upande wa Kakolanya wote wanafanya taratibu za kisheria ili kuachana na tunaweza kufanya mazungumzo ya awali na klabu yoyote ili suala la kisheria likapokamilika basi tutamalizana kabisa.”

 

Pia aliongeza kuwa, kwa sasa wanasubiri majibu kutoka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuhusu barua yao iliyopelekwa na mwanasheria wa Kakolanya kuhusu kuvunjwa kwa mkataba wa kipa huyo. Kakolanya kwa sasa anajifua kama kawa.

MARCO MZUMBE, Dar es Salaam

Comments are closed.