The House of Favourite Newspapers

Meneja Mkuu Global Publishers Aungana na Waombolezaji Kuuzika Mwili wa Shakoor Jongo

0
Meneja Mkuu Global Publishers, Abdallah Mrisho (mwenye kofia katikati) akiwa na waombolezaji katika Makaburi ya Ndugumbi Magomeni Dar es Salaam kwa ajili ya kuuzika mwili wa Shakoor Jongo.
Mwili wa mwanahabari Shakoor Jongo ukiingizwa kaburini.
Waombolezaji wakiweka udongo kwenye kaburi la Shakoor Jongo
Huzuni zikitawala makaburini Ndugumbi wakati mwili wa Shakoor ukizikwa.
Meneja Mkuu Global Publishers, Abdallah Mrisho ameungana na waombolezaji waliojitokeza kuuzika mwili wa Mwandishi nguli wa habari na mdau wa masuala ya burudani, Shakoor Jongo maarufu kama ‘Zungu Fedha’ aliyefariki dunia alfajiri ya leo Septemba 4,2022 baada ya kupata ajali ya gari  katika maeneo ya Meridian Kinondoni jijini Dar es Salaam ambapo mwili huo umezikwa katika makaburi ya Ndugumbi Magombeni.
Zungu aliwahi kuwa mwandishi wa habari Mwandishi wa Global Publishers kupitia magazeti ya Ijumaa, Ijumaa Wikieenda, Risasi na Amani, alikuwa mdau mkubwa wa masuala ya Burudani.
Global Publishers inawapa pole ndugu, jamaa, marafiki na wadau wote wa muziki kwa msiba huo.
Leave A Reply