The House of Favourite Newspapers

Meneja Mpya wa Harmonize Kajala Adaiwa Kumuondoa Mjerumani Konde Gang

0
Kajala Masanja au Mama Paul kuwa C.E.O.

 

OGOPA mno kuchanganya mapenzi na kazi! Saa kadhaa baada ya Harmonize au Konde Boy kumtangaza Kajala Masanja au Mama Paul kuwa C.E.O na meneja wake mpya, meneja mwingine wa jamaa huyo, Beauty Mmari almaarufu Mjerumani anadaiwa kufungasha virago.

Beauty Mmari almaarufu Mjerumani (kulia) akiwa na Harmonize.

 

Katika ukurasa wake wa Instagram, Mjerumani ameondoa utambulisho wa kuwa yeye ni meneja katika lebo hiyo ya Konde Music Worldwide; kwa kifupi Konde Gang.

Jambo hilo limeacha maswali kwa wadau mbalimbali wa muziki kuwa huwenda akawa ameachana na lebo hiyo rasmi baada ya utambulisho wa Kajala.

BONDIA ALIYEWEHUKA ULINGONI AFARIKI, NI YULE ALIYEPIGANA na UPEPO BAADA ya KUCHEZEA KICHAPO

Leave A Reply