The House of Favourite Newspapers

Meta Yazindua Mtandao Mwingine Wa Kijamii Utakaoshindana Na Twitter

0

Kampuni ya META ambayo inamiliki Facebook, Instagram na WhatsApp imezindua mtandao wake mpya uitwao ‘Threads’ mapema wiki hii ikipokea Watumiaji zaidi ya milioni 5 waliojisajili saa nne baada ya kuzinduliwa na mpaka sasa hivi una Watumiaji milioni 10 kwa mujibu wa maelezo ya CEO wa META, Mark Zuckerberg.

Zuckerberg amekubaliana na wazo la kwamba application hiyo mpya itakuwa Mpinzani namba moja wa mtandao wa Elon Musk wa Twitter huku wazo hilo likiwafanya Wakurugenzi Wakuu wa Makampuni hayo makubwa ya teknolojia (Elon na Mark) kusema wat
pambano la ngumi.

Musk amejibu uzinduzi wa mtandao huo mpya kupitia post kadhaa kwenye Twitter akisema “Kheri kushambuliwa na Watu usiowajua kwenye Twitter kuliko kujiingiza katika furaha ya uongo ya kujificha kupitia Instagram”

Watendaji wamesema hakutakuwa na kikomo kwa idadi ya post ambazo Watumiaju wanaweza kuona kwenye threads na mtandao huo utapatikana kwenye zaidi ya nchi 100 kwa Watumiaji wa bidhaa za Apple na Google Play Store.

VIDEO KUTOKA MALAWI: RAIS SAMIA AFIKA KWENYE KABURI la HAYATI KAMUZU BANDA…

Leave A Reply