The House of Favourite Newspapers

Metacha Mnata: Luis, Chama Ni Tishio

0
Metacha Mnata 

MLINDA Mlango wa Yanga, Metacha Mnata, amesema licha ya kuifunga Simba bao 1-0, lakini alikuwa akiomba Luis Miquissone na Clatous Chama wasikae na mpira muda mrefu kutokana na hatari waliyonayo.

 

Chama na Luis wamehusika kwenye jumla ya mabao 13 yaliyofungwa na Simba msimu huu katika Ligi Kuu Bara kati ya 55 kabla ya mechi ya jana dhidi ya Singida United.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Metacha alisema kuwa miongoni mwa vitu vilivyokuwa vikimpa presha ni uwezo wa viungo hao kubadili matokeo muda wowote.

“Ni viungo hatari, tishio, pia wasumbufu ndio maana mipira iliyokuwa miguuni mwao ilikuwa na hatari zaidi, kwangu naona walikuwa na kazi ngumu ya kunitesa nilipokuwa langoni, ila ulinzi niliokuwa nimepewa ulinifanya nikawa bora na mwisho wa siku tukaibuka na ushindi,” alisema Metacha.

 

Katika mchezo huo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Jumapili iliyopita kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar, bao la Yanga lilifungwa kwa faulo ya moja kwa moja na kiungo Mghana, Bernard Morrison dakika ya 44.

DPP AMJIBU LEMA WA CHADEMA, AFAFANUA TUHUMA ZAKE ZOTE – “NAMCHUKULIA HATUA”

Leave A Reply