Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza, James Bwire ameomba nafasi ya kukutana ana kwa ana (appointment) na Rais Dkt. John Pombe Magufuli ili amueleze kinachosababisha malumbano na viongozi wenzake jijini hapo.
Bwire amemueleza hayo Rais Magufuli leo eneo la Igogo, alipopata nafasi ya kuwasalimia wananchi wa Mwanza na kutoa salamu za pongezi kwa rais ambaye yupo ziarani mkoani humo kufungua viwanda na miundombinu mbalimbali ya kiuchumi.
Aidha, akihutubia katika Viwanja vya Nyakato jana, Rais Magufuli aliwataka Meya James Bwire na viongozi wengine wa mkoa huo (ambao hakuwataja) wamalize malumbano yao ili wawatumikie wananchi.