The House of Favourite Newspapers

JPM Azindua Kiwanda cha Dawa, Atoa Wiki 2 kwa Wasioendeleza Viwanda – Video

0
Rais John Magufuli .

RAIS John Magufuli ametoa wiki mbili (siku 14) kuaznia leo kwa wamiliki wa kiwanda cha nguo cha Mwatex cha jijini Mwanza na Kiwanda cha Dawa cha Keko jijini Dar es Salaam kuonyesha mpango madhubuti wa kiutendaji na uendeshaji wa viwanda vyao kinyume cha hilo, viwanda hivyo vitataifishwa na kurejeshwa kwenye umiliki wa umma au kupewa wawekezaji wengine wenye uwezo wa kuviendeleza.

Rais Magufuli amesema hayo leo Jumanne Oktoba 31,2017 alipokuwa akiwahutubia wananchi baada ya kuzindua kiwanda cha dawa za binadamu cha Prince Pharmaceutical eneo la Buhongwa jijini Mwanza.

Amesema Serikali imechoka kusikia kauli za ubabaishaji na maelezo ya “tuko kwenye mchakato” zinazotolewa kama kinga kwa viwanda visivyofanya kazi kwa kiwango kinachostahili. Rais ametoa agizo hilo baada ya kupokea taarifa kuwa Kiwanda cha Nguo cha Mwatex kinafanya kazi kwa asilimia 20 ya uwezo wake wa uzalishaji.

Akizungumzia ujenzi wa kiwanda cha dawa, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema utawezesha mikoa ya Kanda ya Ziwa kuwa na uhakika wa upatikanaji wa dawa kwa bei nafuu na kwamba katika utekelezaji wa Tanzania ya viwanda, wizara kwa kushirikiana na wadau wanakamilisha mchakato wa kujenga kiwanda cha dripu na bidhaa zingine za hospitali mkoani Simiyu.

Kuhusu uboreshaji wa huduma za afya, amesema Mkoa wa Mwanza umepokea zaidi ya Sh7.1 bilioni kwa ajili ya kununua vifaa tiba na dawa wakati jitihada zinaendelea ili kuipatia Hospitali ya Mkoa wa Mwanza ya Sekou-Toure mashine ya CT-Scan.

Leave A Reply