MSTAHIKI Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Benjamini Sitta leo Aprili 30 amezindua rasmi chanjo ya kuwakinga wasichana dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi (HPV) walio na umri miaka 14.
Sitta amesema tatizo la saratani nchini limekuwa likiongezeka na kukua kila mwaka hivyo kusababisha vifo vya wagonjwa wengi kupoteza maisha.
Ameeleza kuwa Serikali imeanza kutoa chanjo hiyo kwa wasichana wenye umri wa miaka 14 ili kuwakinga dhidi ya virusi vya magonjwa ya zinaa ambayo yanasababisha saratani hiyo.
Virusi hivyo vinajulikana kama Human Papilloma Virus (HPV) ambavyo huwaathiri zaidi wanawake. Wataalamu wanasema idadi kubwa ya wanawake wanakufa kutokana na ugonjwa huo kwa sababu ya kutoutambua mapema.
Comments are closed.