The House of Favourite Newspapers

Mfahamu T.B Joshua

0

HABARI za kifo cha Temitope Balogun Joshua ambaye ni maarufu kwa jina T.B Joshua zimewashtua watu wengi Nigeria na dunia kwa ujumla.

Kanisa lake la Sinagogi la mataifa yote maarufu SCOAN ambalo lilianzishwa na muhubiri huyo lilithibitisha habari za kuhuzunisha za kifo chake Jumapili alfajiri likisema:.

 

“Mungu amemchukua mtumishi wake kama inavyostahili kwa upako. Nyakati zake za mwisho zilikuwa katika kumtumikia Mungu. Alizaliwa, kuishi na kufariki akitimiza hilo”, zimeandika zilizokuwa kurasa zake za mitandao ya kijamii.

Mfahamu T.B Joshua

Muhubiri TB Joshua ni raia wa Nigeria Mwanzilishi huyo wa Kanisa la Synagogue Church of All Nation (SCOAN) na Kituo cha Televisheni cha Emmanuel (Emmanuel TV)ambalo limekuwa likirusha matangazo yake mubashara katika runinga ya  mjini Lagos kusini mwa Nigeria.

 

T.B Joshua Alizaliwa kama mwezi  June 12, 1963,  katika jimbo la Ondo nchini Nigeria.

 

Kulingana na Mtandao wa kanisa lake la SCOAN , Joshua alikuwa ndani ya tumbo la mamake kwa miezi 15 kabla ya kuzaliwa kwake tofauti na miezi tisa ambayo imezoeleka.

 

Joshua alisomea katika shule ya msingi ya St. Stephen Anglican {Ikare-Akoko, Nigeria 1971-1977} lakini aliwacha shule baada ya mwaka mmoja na kufanya kazi katika shamba moja la kuku.

 

kwa Mujibu wa Mtandao wa SCOAN akiwa shuleni alijulikana kama muhubiri mdogo kutokana na alivyokuwa akiipenda Biblia na uwezo wa kutabiri matukio yaliofanyika katika jamii yake ,

 

Alianzisha kanisa la SCOAN mwaka 1987 akiwa na waumini wachache kabla ya kanisa hilo kukua na  kupanuka hadi kimataifa.

 

Mwaka 2009 TB Joshua ambaye alijulikana kwa kupenda mchezo wa soka, alianzisha klabu ya kandanda kwa jina My people FC katika juhudi za kuwasaidia vijana.

 

Wachazaji wawili wa timu hiyo Sani Emmanuel na Ogenyi Onazi walichezea Nigeria Golden mwaka 2009, katika kombe la dunia la wachezaji chimi ya miaka 17, Tayari wachezaji watatu wamepata ufadhili Ulaya kuwa wachezaji wa kulipwa nchini Sweden.

 

Kulingana na jarida la Forbes 2011 , Temitope Joshua ni muhubiri wa tatu tajiri nchini Nigeria akiwa na thamani ya $15m.

Leave A Reply