The House of Favourite Newspapers

Mfalme wa Thailand Amvua Mkewe Umalkia

MFALME wa Thailand, Vajiralongkorn,  ametangaza kumvua vyeo vyake vyote mke wake kutokana na tabia mbaya na kutokuwa mwaminifu kwa ufalme.

Sineenat Wongvajirapakdi, mke wa nne aliteuliwa mwezi Julai ikiwa ni miezi miwili tu baada ya mfalme Vajiralongkon kumuoa Queen Suthida.

Tangazo rasmi la Serikali lilisema kuwa Sineenat alikuwa mwenye tamaa na alijaribu kujiweka katika hadhi ya malkia.

“Tabia hiyo ya  mke wa mfalme zilichukuliwa kama ukosefu wa heshima,” ilisisitiza taarifa hiyo.
Kwa mujibu wa Shirika la habari la Reuters, Sineenat ambaye alikuwa meja-jenerali na rubani wa ndege za kivita, muuguzi na mlinzi alikuwa mtu wa kwanza kutunukiwa cheo cha mke Mtukufu wa Ufalme.

Malkia Suthida mwenye umri wa miaka 41 ambaye alikuwa mhudumu wa zamani wa ndege na naibu mkuu wa kikosi cha walinzi wa kifalme,  alikuwa mpenzi wa muda mrefu wa Mfalme Vajiralongkorn.

 

Inaelezwa kuwa miaka mingi mara kwa mara amekuwa akionekana kando ya Mfalme Vajiralongkorn na aliaminiwa kuwa ndiye mtu aliyekuwa karibu naye kuliko mtu mwingine lakini sasa amevuliwa rasmi cheo hicho.

 

Habari zaidi zinasema kuwa hata baada ya kumuoa Malkia Suthida, bado Sineenart alikuwa ndiye mtu aliyeonekana zaidi na kuheshimika katika matukio ya kifalme.

 

Tangazo la kuvuliwa vyeo kwa Sineenat lilichapishwa katika jarida la Ufalme Jumatatu iliyopita na kueleza kuwa kuanguka kwake kutoka cheo cha juu katika ufalme wa Thailand ni mabadilikoya ghafla ya hadhi yake ya juu aliyokuwa nayo ndani ya Ufalme.

 

Sababu za kung’olewa
Tangazo hilo lilisema “alionyesha pingamizi na shinikizo kwa njia zote katika kuzuia uteuzi wa Malkia kabla ya harusi ya mwezi Mei.

Tangazo hili lilisema kuwa mwanamke huyo alionyesha upinzani dhidi ya Mfalme na Malkia na kukiuka mamlaka kwa kutoa amri kwa niaba ya mfalme.

“Tulibaini kuwa hakuwa mwaminifu kwa mamlaka aliyopewa na wala hakuwa na maadili yanayofaa kulingana na hadhi yake,” lilisema tangazo.


Hata hivyo, wachunguzi wa masuala ya siasa nchini humo wansema sababu ya kweli ya kuanguka kwa Sineenart huenda isiwekwe wazi kwa umma ikizingatiwa usiri unaotawala masuala ya kasri ya Ufalme wa Thailand.

Sheria ya Ufalme inayozuia kuutukana ufalme ni miongoni mwa sheria kali zaidi duniani lakini kuvuliwa mamlaka kwa Sineenat kunafanana na yale yaliyowakuta wake wawili wa zamani wa mfalme huyo.

Mfalme Vijiralongkor ni nani?

Vajiralongkor alitawazwa kuwa mfalme baada ya kifo cha baba yake mwaka 2016. Ameoa wake wanne akiwamo Malkia Soamsawali aliyefunga naye ndoa mwaka 1977, Yuvadhida Polpraserth, Srirasmi Suwadee na Mfalme Suthida.

Mwaka 1996 alimkataa mke wake wa pili ambaye ilibidi atorokee Marekani ambako amekuwa akiishi tangu wakati huo na akawakataa watoto wake wanne aliozaa naye.

Mwaka 2014 mke wake wa tatu Srirasmi Suwadee pia alivuliwa vyeo vyake vyote na kusababisha mtoto wake mvulana mwenye umri wa miaka 14 kulelewa nchini Ujerumani na Uswiss.

Comments are closed.