The House of Favourite Newspapers

Mfanyabiashara Krushna Karia Afutiwa Kesi na Mahakama ya Kisutu

0
Mfanyabishara kutoka jijini Mwanza Krushna Karia (katikati) akiwa  na wakili wake, Raymond  Uisso wakitoka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mara baada ya kufutwa kwa kesi hiyo.

 

MFANYABIASHARA, Krushna Karia (37) Mkazi wa Makoroboi jijini Mwanza, amefutiwa mashtaka yake katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa ambapo alikuwa akikabiliwa na tuhuma za wizi wa vitu mbalimbali vyenye thamani ya Sh milioni 284.8 alivyopewa na Kiwanda cha Cello kwa malengo ya kibiashara.

Mashtaka hayo yamefutwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi ambapo kesi hiyo ilikuwa imekuja kwa ajili ya kutajwa na upande wa mashtaka kuieleza Mahakama kuwa DPP ameamua kutokuendelea na kesi hiyo.

Leave A Reply