The House of Favourite Newspapers

Mfumo wa BOLT Ulivyowanufaisha Watanzania

0

 

“Nafurahia zaidi uhuru ninaopata kufanyakazi kupitia mfumo wa Bolt. Nina uhuru wa kufanya kazi masaa ninayotaka na wakati ninaotaka.

 

Nilianza udereva na Bolt nilipokuwa nasoma chuo na shughuli hii imeniwezesha kujikimu kimaisha. Nimeweka akiba ya hela kwa mipango ya kuanzisha biashara ya duka la vifaa vya ujenzi nikishirikiana na marafiki zangu.

 

Mfumo wa usafiri kupitia mtandao ni nafuu na abiria wanaweza kusafiri kwa raha bila kumiliki usafiri binafsi.

 

Ninashauri vijana leo kuwa na ujasiri na wasiogope kuanza na kujaribu vitu vipya ambavyo vinaweza kuwainuakimaisha. Ninajivunia kile nilichofanikiwa mpaka sasa.

 

Nilianza kuendesha gari kwa mkataba na kampuni na niliweza kuweka akiba ya kutosha kununua gari langu mwenyewe. Mfumo wa usafiri wa mtandao kupitia Bolt umechangia sehemu kubwa katika mafanikio yangu ”Dereva Bolt, Jeremiah Laurence Salufu (27), Salasala – Dar es Salaam.

Leave A Reply