The House of Favourite Newspapers

NMB Yawa ya Kwanza Kutekeleza Rasmi Mpango wa Ushirika Afya

0
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kasimu Majaliwa (kulia) akimkabidhi kadi ya bima ya afya mkulima wa tumbaku – Kulwa Mfaume kutoka chama kidogo cha ushirika Kabungu Wilaya ya Kaliua Mkoani Tabora.

 

Benki ya NMB imekuwa taasisi ya kwanza kutekeleza rasmi mpango wa bima ya afya kwa wakulima nchini baada ya kuingia makubaliano ya kutoa huduma hiyo na vyama vikuu viwili vya ushirika mkoani Tabora, ambavyo ni WETCU na MILAMBO vinavyowakilisha vyama vidogo vya wakulima zaidi ya 200 mkoani humo.

 

Kupitia mpango wa Ushirika Afya wanachama wa vyama hivyo wapewa mikopo isiyo na riba na Benki ya NMB kwa ajili ya gharama za matibabu kwa kutumia kadi za NHIF. Utiaji saini wa makubaliano hayo na vyama vya wakulima wa zao la tumbaku yanayouhusisha pia Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ulifanyika Tabora kama sehemu ya kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Ushirika.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania – Kasimu Majaliwa (kulia) akimkabidhi kadi ya bima ya afya mkulima wa tumbaku – Atanas Gabriel  kutoka kikundi cha ushirika Urambo  Wilaya ya Urambo  Mkoani Tabora. 

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa alizindua rasmi mpango huo kwa kuwakabidhi kadi za NHIF wakulima wa tumbaku; Kulwa Mfaume, Saleh Mpemba na Athanas Semeduke ambao ni miongoni mwa kadi 102 za kwanza ambazo zimetolewa na benki hiyo. Lakini pia kadi 90 zitatolewa kwa wakulima mkoani Kahama.

Vilevile, aliishukuru NMB kwa mchango wake wa kuviimarisha vyama vya ushirika na kuvifanya kuwa nguzo muhimu ya kiuchumi.

Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB,Filbert Mpozi (wa pili toka kulia) Mwenyekiti  wa WETCU ,Hamza Rajabu wa pili kutoka kushoto,  mwenyekiti chama cha  ushirika  cha Milambo John Ntezilyo na kulia kabisa ni Mkurungenzi Mkuu wa mfuko wa Bima ya Taifa ya afya (NHIF),Benard Konga wakionyesha  mkataba  wa mikopo wa bima ya afya kwa wakulima waliosaini na vyama vikuu vya ushirika vya WETCU na MILAMBO mkoani Tabora.

 

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo, Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB, Bw. Filbert Mponzi alisema, NMB imetenga zaidi ya TZS bilioni 5 kwa ajili ya kuwakopesha wakulima chini ya utaratibu wa Ushirika Afya. Lakini pia wana mpango wa kuongeza kiasi cha pesa ili kuwafiki wakulima zaidi ya 300,000 nchi nzima.

 

Utaratibu huu utarahisisha kazi ya kuwahamasisha wakulima kijiunga na vyama vya ushirika na utaongeza idadi ya watu wenye bima za afya kama serikali inavyotaka na kuelekeza.

Leave A Reply