The House of Favourite Newspapers

Mgombea Ubunge Zanzibar, Turky Afariki Dunia

0

 

ALIYEKUWA Mbunge wa Jimbo la Mpendae Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia alikuwa anatetea kiti chake kwa sasa, Salim Hassan Abdullah Turky, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo, Septemba 15, 2020, katika Hospitali ya Tasakhta Global baada ya kuugua ghafla.

 

Salim Turky ambaye alizaliwa Februari 11, 1963, alikuwa mwenyekiti wa makampuni ya Turky ambapo chini yake yalikuwa makampuni 12 yanayoendesha biashara zake Tanzania Bara, Zanzibar na visiwa vya Comoro.  Baadhi ya makampuni hayo yanajumuisha Hoteli ya Golden Tulip, Hospitali ya Tasakhtaa Zanzibar, biashara za saruji,  na biashara za vyakula na mafuta.

 

Mwanasiasa huyo mkongwe ambaye pia alikuwa maarufu kwa jina la Mr. White anatarajiwa kuzikwa alasiri ya leo, Septemba 15, 2020, katika Makaburi ya Fumba, Zanzibar.

 

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na familia ya marehemu, Turky ambaye amekuwa Mbunge wa Mpendae tangu  2010 ataswaliwa alasiri ya leo katika Msikiti wa Othman Maalim na kufuatiwa na mazishi.

 

Enzi za uhai wake amewahi kunukuliwa akisema:

“Nataka kuiweka Tanzania sehemu salama na ya ukweli, maneno mengine si sawa kurushiana tusifanye tukio la Lissu kutaka kufanya siasa mimi binafsi tukio la Lissu limenisononesha sana na kunisikitisha. Mimi ni binadamu ambaye naamini kuna kuzaliwa na kufa.

 

“Mimi nilitumia uwezo niliojaliwa na Mungu nikatafuta ndege kwa ‘Flight Link’ ambao ni ndugu zetu tunafanya nao biashara sana wakakubali kutusaidia kwa dola 9,200, ile ndege mimi ndiyo niliiita kwa kukubaliana na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbow,e kwamba nisimamie mambo hayo baadaye wao waje kurejesha na ndicho kilichotokezea.”

 

Leave A Reply