The House of Favourite Newspapers

Mgombea urais wa Zanzibar Dk Shein aendelea na mikutano yake ya kampeni Zanzibar

0

Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM Dk Ali Mohamed Shein, akiwahutubia Wananchi na Wanachama wa CCM katika viwanja vya garagara mtoni akiwa katika mikutano yake ya kampeni ya kugombea Urais wa Zanzibar. kwa kupata ridhaa za Wananchi kuongoza Zanzibar kwa Maendeleo ya Wananchi wa Zanzibar katika sekta mbalimbali na kudumisha Amani na Utulivu katika Visiwa vya Unguja na Pemba.

Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM Dk Ali Mohamed Shein, akimtambulisha Mgombea Ubunge wa Jimbo la Welezo Zanzibar kupitia CCM Saada Mkuya katika viwanja vya garagara mtoni Zanzibar.

Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Dk Ali Mohamed Shein, akimtambulisha Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mtoni Zanzibar wakati wa mkutano wa kampeni za Urais wa Zanzibar Dk Shein katika viwanja vya garagara mtoni Zanzibar.

Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, akimtambulisha Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mfenesini Zanzibar Kanali Mstaaf Khamis , wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya garagara mtoni Zanzibar.

Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, akiwatambulisha Wagombea Uwakilishi wakati wa mkutano wa kampeni za Urais zilizofanyika katika viwanja vya garagara Zanzibar.

Mama Fatma Karume akiwahutubia Wananchi wakati wa mkutano wa Kampeni ya Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. Ali Mohamed Shein, uliofanyika katika viiwanja vya Garagara mtoni Zanzibar na kuwataka siku ikifika kutia kura ya Ndio kwa Dk Ali Mohamed Shein.

Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohameid Shein, akisalimiana na Mama Fatma Karume alipowasili katika viwanja vya garagara mtoni kwa ajili ya mkutano wake wa kampeni.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Magharibi Ndg Yussuf Mohammed akizungumza na Wananchi na WanaCCM katika viwanja vya garagara mtoni wakati wa mkutano wa kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, na kuwatana Wananchi kumpigia kura Dk Shein, ili kuzidi kuleta maendeleo katika Visiwa vya Unguja na Pemba katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein. akisalimiana na Viongozi wa CCM alipowasili katika viwanja vya garagara mtoni kwa ajili ya kuendelea na mikutano yake ya kampeni Zanzibar kuomba ridhaa za Wananchi kumchagua tena kuongoza Zanzibar.

Wasaani wa Bendi ya Moto wakitowa burudani kuhamasisha Wanachama wa CCM wakati wa mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, zilizofanyika viwanja vya garagara mtoni Zanzibar.

Wanachama wa CCM wakiwa katika viwanja vya garagara wakihudhuria mkutano wa kampeni ya mgombea wa Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein.

Wanachama wa CCM wakishangilia wakati wa mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urai kupitia CCM katika viwanja vya garagara Mtoni Zanzibar.

Wanachama wa CCM wakishangilia wakati wa Mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya garagara mtoni Zanzibar na kutowa sera za CCM kwa kipindi cha miaka mitano ijayo ya kipindi chake baada ya kupata ridhaa za Wananchi kumpa kura ya Ndio.katika uchaguzi mkuu mwa huu.

Leave A Reply