The House of Favourite Newspapers

Mgomo Mzito Wa Madereva Wa Tanzania Waliopo Congo DRC Wahamasishwa, Anayekaidi Kukiona

0
Mwenyekiti wa TAMSTOA, Chuki Shabani (katikati) akizungumza kwenye mkutano na wanahabari leo, kushoto ni Katibu Mkuu wa chama hicho, Issa John na kulia ni makamu mwenyekiti wa chama hicho, Mgendela Gama.

Dar es Salaam 4 Novemba 2023: Madereva wa malori wa Tanzania waliopo nchini Congo DRC wako kwenye wakati mgumu baada ya kuhamasishwa kuwafanyia mgomo mabosi wao ili wawape posho iliyotajwa na kinara wa mgomo huo kama ‘Risk Allowance’ ambayo amesema hiyo ni posho ya kimataifa ulimwengu mzima hivyo nao wanahitaji wapewe.

Akizungumza na wanahabari kwenye Hotel ya Double View iliyopo Sinza jijini, Mwenyekiti wa Wamiliki wa Malori nchini (TAMSTOA), Chuki Shabani aliyekuwa na kamati ya chama hicho amesema posho hiyo inayodaiwa kuwa ya kimataifa wao hawajawahi kuisikia. Aliendelea kusema;

“Kuna mtu mmoja tunasikia anaitwa Steve ambaye tumemfuatilia na kupata mpaka namba ya hati yake ya kusafiria ndiye kinara wa kuhamsisha mgomo huo kwa kuwataka madereva wote kupaki malori waliyokabidhiwa mpaka watumiwe posho hiyo na mabosi wao.

“Jambo analofanya ni huyu jamaa ni baya sana na mbaya zaidi imesemwa kwamba kama kuna dereva ataamua kukaidi mgomo huo wamepanga kumshambulia huyo dereva na hiyo gari anayoendesha”.

Kufutia hali hiyo mwenyekiti huyo ameiomba serikali kupitia kitengo cha kuzuia uhalifu wa mitandaoni ‘Cibercrime’ kumfuatilia na kumkamata mualifu huyo anayechochea mgomo kupitia mitandaoni na kumfungulia mashitaka.

Chuki amesema wao kama walipa kodi kufuatia mgomo huo serikali inapoteza mapato mbalimbali kama vile ushuru wa bandarini, ununuzi wa mafuta na mengineyo.

Hivyo serikali tunaomba itusaidie kumdhibiti mharifu huyo anayetoka hapa nchini ambaye anayetaka kutuvuruga. Alimaliza kusema Chuki Shabani na kuungwa mkono na Makamu wake Mwenyekiti Mgendela Thobias Gama.

Leave A Reply