The House of Favourite Newspapers

Mgunda: Tunaanza Upya leo Dhidi ya Geita Gold CCM Kirumba jijini Mwanza

0
Kocha Mkuu wa Simba, Juma Mgunda.

KUELEKEA mchezo wao wa kwanza wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Geita Gold unaotarajiwa kupigwa leo Jumapili, Kocha Mkuu wa Simba, Juma Mgunda, ameweka wazi kuwa, hawaangalii historia ya matokeo ya mzunguko wa kwanza.

Mgunda alibainisha kwamba, kwa sasa wanapiga hesabu pointi 45 za mzunguko wa pili katika mechi 15 ili kuwania ubingwa baada ya mzunguko wa kwanza kukusanya 34.

Leo Jumapili, Simba wanatarajiwa kuwa wageni wa Geita Gold katika mchezo wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, ambapo huo unakuwa mchezo wa kwanza kwa Simba kwenye mzunguko wa pili.

Simba wataingia katika mchezo wa leo wakiwa na kumbukumbu nzuri ya kuibuka na ushindi wa mabao 0-3 katika mchezo wa mwisho ugenini dhidi ya Coastal Union. Wamemaliza mzunguko wa kwanza wakiwa na pointi 34 baada ya mechi 15.

Akizungumza na Spoti Xtra, Mgunda alisema: “Tulikuwa na wakati mzuri katika michezo yetu ya kumaliza mzunguko wa kwanza kwa kushinda michezo miwili ya ugenini, lakini tunafahamu mchezo huu utakuwa mgumu zaidi.

“Hivyo tutaingia katika mchezo huu kwa kuanza upya hesabu zetu kuhakikisha tunashinda kila mchezo, ili kufikia malengo yetu msimu huu.”

STORI: JOEL THOMAS

”SIMBA TUNAIJUA NJE NDANI, HAWAAMINI KIKOSI CHAO” – SHOMBO ZA MASHABIKI WA YANGA…

Leave A Reply