TEMBA KAFUNGUKA USIYOYAJUA KUHUSU CHEGE, BI CHEKA KUSEPA TMK – VIDEO

MMOJA wa malejendari ya Bongo Fleva, Amani Temba ‘Mheshimiwa Temba’ leo alitua ndani ya Studio za +255 Global Radio zilizopo Sinza-Mori jijini Dar na kufunguka ishu mbalimbali baada ya kupotea kwa kitambo kirefu.

 

Kupitia +255 Global Global Radio (GR), Temba alifunguka juu ya ngoma zake mpya za Mtaalam wa Dar na Kulikoni, ungana naye;

GR: Vipi kuhusu TMK Wanaume family, ilianzia wapi?

 

Temba: Nilipojiunga na TMK ilikuwa ngumu kwa sababu ya kazi yangu ya jeshi, lakini baadaye nilijiunga na wenzangu baada ya kundi kusimama na mishemishe zangu kuzingua. Nakumbuka mmoja wa waanzilishi wa TMK Wanaume mbali na Juma Nature na KR pia alikuwepo Swebe Santana (mwigizaji).

GR: Vipi kuhusu Bibi Cheka?

Temba: Sijawasiliana naye muda mrefu, lakini aliondoka kwa sababu zake na hatukuwa tumeandikiana hivyo ana haki ya kusema chochote.

 

GR: Vipi kuhusu kombinesheni ya Chege na Temba? Mbona siku hizi haisikiki?

Temba: Joint ya Temba na Chege ilipendwa na kila mtu akiwemo Mam aliyekuwa msambazaji wa nyimbo zetu wakati wa Twende Zetu. Hatuna shida, tupo pamoja, tunasalimiana, sema ndiyo hivyo maisha yanabadilika kutokana na majukumu, lakini hakuna shida.

GR: Vipi Mkubwa na Wanawe?

Temba: Kuhusu kuanzishwa kwa Mkubwa na Wanawe, mimi ndiyo nilikuwa nimelala nikapata wazo. Nilimfuata Said Fella, nikamwambia watu wanasema unadhulumu wasanii, lakini mimi nilikuwa sioni kama anadhulumu. Lakini nilimwambia Fella tuanzishe kitu kama hicho na kweli tulifanikiwa kuanzia kwa Aslay na wengine ambao tuliwafungulia njia. Hiyo niliona ni njia bora ya kuondoa ile mentality (dhana) kwamba anawadhulumu watu, lakini huwezi kumnyima mtu kusema na kama mtu anadhulumiwa ana haki ya kusema, lakini lengo letu lilikuwa ni kupeleka muziki wetu mbali.

 

GR: Je, upo tayari kufanya kolabo na madogo wa Yamoto?

Temba: Hawawezi kukataa, ni wadogo zangu na wakikataa watakula makozi (utani).

GR: Nini sababu ya kuweka kijiti mdomoni muda wote?

Temba: Nimetoka kupiga msosi hapo jirani (utani)…naweza kusema ni stahili yangu na kila mtu anashangaa hadi kuna watu wanajua ninalala nacho. Nipo mbioni kuanzisha brandi yangu ya vijiti, lakini nyingine ni bransi ya sabuni zangu.

GR: Ngoma ya Mtaalam wa Dar idea ilikujaje?

Temba: Nilimsikiliza Rais wetu (Magufuli) akizungumza namna tulivyokuwa tunapigwa kwenye mambo mbalimbali yakiwemo madini, mikataba mibovu na ishu nyingine kama hizo nikaona niiandikie ngoma baada ya kumsikiliza mheshimiwa ndiyo maana unasikia kuna sehemu ninataja maeneo kama Mirerani kwenye madini ya Tanzania.

GR: Kwa nini ngoma zako hazina views nyingi kwenye YouTube?

 

Temba: Ni kweli nilichelewa kidogo, lakini ngoma zipo na zinakimbiza kama mtu anataka kuziona ni kuzicheki tu.

GR: Nini siri ya kuwa na identity kama ilivyo kwa wasanii wengi wa zamani?

Temba: Ilikuwa ni lazima kuwa na identity yako na ilikuwa ukijifanya wewe kama mtu mwingine ilikuwa unapigwa chupa. Hawa wa siku hizi wanafanana, lakini bado wanapiga hela na wanapendwa na wako sawa.

GR: Zamani mlikuwa mnaandika ujumbe sana, lakini siku hizi haiko hivyo, je, nini mtazamo wako?

Temba: Hawakosei, kila kipindi kina vitu vyake kila kitu kina wakati wake. Ukitaka kushindana na wakati utalamba mchanga. Cha kufanya wewe ni kukimbizana nao na kitu kikawa mwake, mwakemwake baba’ke.

GR: Muziki unaendesha maisha yako kwa kisai gani?

Temba: Ni fifty-fifty (hamsinihamsini), siwezi kuacha muziki kwani ndiyo utambulisho wangu na umenitoa mbali.

GR: Nini kimetokea kati ya TMK Wanaume na East Coast Team (Ay, Mwana-FA na GK)? Hatujawahi kuona kolabo!

Temba: Hakuna tatizo hata kidogo, tulishafanya kolabo huko nyuma na ni washkaji zetu hatuna tatizo kabisa, tupo poa sana.

 

GR: Umefanya kazi na maprodyuza wengi kama Master Jay na P Funk Majani, unawazungumziaje maprodyuza wapya?

Temba: Ni kweli nilifanya nao wote, lakini zaidi ni Master Jay ambaye amefanya kazi zangu nyingi. Lakini ninawakubali sana maprodyuza wengine wengi wanafanya poa sana.

GR: Wewe ni mmoja wa wasanii waliokuwa wanaandika ngoma zenye ujumbe tata lakini kwa sasa hatuzisikii?

Temba: Siwezi kumsemea mtu, lakini mimi nimebadilika kwa sababu hii ni nchi na ina taratibu zake hivyo nimebadilisha na kufuta baada ya mistari kwenye ngoma zangu.

GR: Una mpango wa kufanya kolabo na wasanii wa kike kama ulivyofanya na Ray C?

Temba: Nimeshafanya nao sana. Nimefanya na dada mmoja yupo Twanga Pepeta anaitwa Fetty na wengine kama Katrina.

GR: Unawaahidi nini mashabiki wako?

Temba: Nilisema mwaka huu ni back to back so baada ya ngoma zangu mbili, soon baada Mtaalam wa Dar na Kulikoni hivyo wakae tayari kupata pini baada ya pini.

 

SIKILIZA GLOBAL RADIO

Jinsi ya kuipata +255 Global Radio ingia kwenye Mtandao wa www.globalpublishers.co.tz halafu kwa juu utaona pameandikwa LISTEN LIVE ukibonyeza hapo utakuwa umeipata. Kwenye instagram akaunti ya +255globalradio kwa juu utabonyeza link kwenye bio. Hata ukiwa na MB 50 utakula ngoma kwa saa kibao.

 

 

 

Loading...

Toa comment