The House of Favourite Newspapers

Shabiki wa Real Madrid, Kula Eid na Mamilioni ya M-Bet

 KAMA ni zali,  basi limemwangukia shabiki wa Real Madrid, Gadi Majweka,  mkazi wa Morogoro ambaye atakula Sikukuu ya Eid bila ya mawazo baada ya kushinda kiasi cha Sh. milioni 208 kutoka kampuni ya Michezo ya Kubashiri ya M-Bet.


Gadi ambaye ni mfanyabiashara wa rangi za mikeka ameshinda kiasi hicho cha fedha baada ya kubashiri kwa usahihi timu 12 kwa kucheza Perfect 12 ya M-Bet.

Akizungumza na waandishi wa habari, Gadi amesema kwamba imemchukua miaka mitatu kushinda kiasi hicho cha fedha ambacho ameshinda na Perfect 12 ya M-Bet, ambapo kwa muda wote huo alikuwa anacheza kwa kila siku.


“Nimefurahi kushinda fedha hizi ambazo ni kiwango kikubwa kwangu kushinda. Huko nyuma nilikuwa nashinda laki lakini sikuwahi kushinda hii Perfect 12.

“Nawashukuru M-Bet na baada ya kushinda nitakuwa Mr Perfect huko kwetu, hadi nashinda nimekuwa nikicheza kwa miaka mitatu mfululizo, ninacheza kila siku asubuhi, mchana na hadi usiku,” alisema Gadi.


Naye Ofisa Masoko wa M-Bet, Allen Mushi,  amesema M-Bet bado wataendelea kutoa dau zaidi kwa kila mshindi ambaye atashinda Perfect 12.

“Dau la Perfect 12 kila siku linapanda, ninawaambia tu watu waendelee kucheza Perfect 12 na sisi tutatoa kwa washindi wote. Huyu ni mshindi wa tano wa Perfect 12 kwa mwaka huu na tutazidi kutoa zaidi na zaidi,” alisema.

Comments are closed.