The House of Favourite Newspapers

Miaka 15 ya Saida Karoli Kwenye Game ya Muziki (Pichaz +Video)

0
Msanii wa nyimbo za asili, Saida Karoli, alipopanda stejini kwa mara ya kwanza katika shoo iliyofanyika Escape One, Mikocheni Dar, usiku wa kuamkia leo.

MWIMBAJI wa nyimbo za asili Bongo, Saida Karoli, usiku kuamkialeo amefanikiwa kukusanya umati wa Watanzania katika Ukumbi wa Escape One, Mikocheni, jijini Dar es Salaam waliokuwa wamem-miss kwa muda mrefu tangu alipopotea kwenye gemu ya muziki.

Shoo hii iliyofanyika ilipewa jina la Kunyanyuka, Kuanguka na Kusimama Tena. Saida aliyekuwa amepotea kwa muda mrefu amesimama tena na amerudi tena akiwa na ngoma mpya ambayo imependwa na watu wengi inayoitwa Orugambo.

Mmiliki  wa Jembe ni Jembe, na Mkurugenzi wa Jembe FM Radio, Dr Sebastian Ndege, amewaomba Watanzania wote kumuunga mkono Saida Karoli kwa kuposti wimbo wake kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.

“Tutahakikisha Saida Karoli anastawi na kufikia ngazi za kimataifa,” alisema Ndege akiwataka pia mashabiki wamuunge mkono msanii huyo kwa kununua CD za nyimbo zake.

Tamasha hilo lilihudhuriwa na Waziri wa Habari na Utamaduni, Harrison Mwakyembe, aliyesema serikali inatambua mchango wa Saida wa kutangaza nyimbo za asili kwa muda mrefu na alisema serikali itaendelea kumsapoti.  Pia wabunge na wasanii mbalimbali walifika kutoa mkono wao wa kumsapoti msanii huyo aliyewika miaka ya nyuma.

Saida aliwavutia mashabiki wake kwa kuimba akiwa na mawazi tofauti katika awamu tatu alizokuwa anatoa burudani ukumbini hapo, jambo lililowafanya mashabiki kuinuka kwenye viti vyao na kucheza huku wakimtunza ‘mapesa’.

Msanii huyo aliwashukuru Watanzania na kamati nzima iliyomwandalia shoo hiyo kwa kumuunga mkono na kuwaomba mashabiki wote wampokee upya kwani ana vitu vipya vya kuwapa.

Baadhi ya wasanii waliomsindikiza Saida Karoli ni Dito na vijana kutoka THT.

Kupata uhondo wa shoo hii kuanzia mwanzo mpaka mwisho angalia video ya Global TV iliyokuwepo ukumbini hapo ikikuletea tukio hilo mubashara.

…Akitoa burudani. 

Sura kamili ilivyokuwa ukumbini ambapo Saida na wanenguaji wake walipokuwa wanajituma na kutoa burudani ya kukata na shoka kwa watu wote waliofika hapo.

(PICHA: MUSA MATEJA/GPL)

Leave A Reply