The House of Favourite Newspapers

Michirizi Ya Damu – 05

0

Hakutaka kubaki nyumbani, akaelekea huko na kuonana na mwanaume huyo na kumfanyia kituko cha kumshika katika zipu yake. Godfrey akachanganyikiwa lakini akamwambia kwamba angempigia simu.

 

Hakutaka kujifanya kuwa na haraka, alijua kwamba mwanaume huyo angekuwa na presha ya kuonana naye, alitaka kuvuta muda mpaka wiki moja iishe ndiyo awasiliane naye.

 

Wakati akisubiri wiki moja ipite, akaanza kupata madili mengi, akawa mtu wa kuzunguka nchi mbalimbali kufuata wateja kiasi kwamba mpaka miezi yote hiyo inakatika bado alikuwa bize na wateja hao, na aliporudi Tanzania, mtu aliyemjia kichwani mwake alikuwa Godfrey hivyo kumpigia na kuonana naye kisha kufanya kile kilichowafanya wapigiane simu.

 

“Wewe ni zaidi ya wapenzi wangu wote,” alisema Fareed.
“Kweli?”
“Haki ya Mungu tena. Ninakupenda sana mpenzi! Hakika sijuti kuwa nawe,” alisema Fareed, akachukua mkoba wake, akatoa wanja na kuanza kujipaka vizuri huku akijiangalia kwenye kioo.

“Ninafurahi sana kukutana nawe. Hakika sitokuacha. Nitakuwa radhi kuachana na mke wangu ila si kukuacha wewe,” alisema Godfrey huku akionekana kuchanganyikiwa. Kwa kifupi ni kwamba akatekwa na penzi jipya.

****

Hali ilibadilika, mapenzi ya Godfrey kwa mkewe yakapungua, hakutaka kuwa naye karibu kama ilivyokuwa siku za nyuma, mapenzi yalikuwa kwa mwanaume tata ambaye alikutana naye ufukweni.

Walikuwa wakiwasiliana kama kawaida, mara kwa mara walikutana na hata alipokuwa akienda safari zake za Ulaya, Marekani na nchi nyingine alikuwa akiongozana naye ambapo huko uchafu wao uliendelea.

Fareed aliendelea kufanya mambo yake kama kawaida, alimpenda sana Godfrey, alimpa kila kitu alichotaka lakini siku zote alitamani kutembea na wanaume wengine. Aliijua dunia, alijua nchi zilizokuwa na wanaume tata wengi, watumiaji wa watu hao na hata alipokwenda huko, wakati mwingine alikuwa akimtoroka Godfrey na kujiunga na wenzake kufanya ufuska.

Siku ziliendelea kukatika, walipokuwa wakirudi nchini Tanzania, halikuwa jambo la ajabu kumuona Godfrey akiondoka nyumbani na kurudi baada ya siku tatu. Kila alipokuwa akiulizwa, alikuwa mkali, aligombana na mkewe kisa tu alihisiwa kulala na wanawake wengine.

Mkewe akaanza kupeleleza, aliamini kwamba kwa namna moja au nyingine ilikuwa ni lazima kuwe na mwanamke aliyekuwa akimzuzua mume wake hivyo kumfuatilia.

Alifuatilia kwa kuchukua simu yake nyakati za usiku na kuangalia meseji mbalimbali, hakuweza kugundua, hakuacha, aliendelea kufuatilia watu aliokuwa akiwasiliana nao, wengi walikuwa wanaume lakini kulikuwa na mwanaume mmoja ndiye aliyekuwa akiwasiliana naye sana, huyu aliitwa Fareed.

Mara ya kwanza akahisi kwamba alikuwa msichana aliyembadilisha jina, akaangalia katika mtandao wa simu kwenye huduma ya kifedha kugundua kama hilo lilikuwa jina lake au mumewe alimfanyia mchezo, alipoangalia, akakutana na jina hilohilo, Fareed Hassan.

Hakuwa na hofu na mwanaume huyo, aliendelea kutafuta lakini hakumfuma mumewe kuwa na uhusiano wa siri na mwanamke mwingine. Akauachia moyo wake kumwamini mwanaume huyo, akajiondoa hofu, akaona kwamba kila alipokuwa akiambiwa kwamba alikuwa bize na mambo ya biashara, kweli alikuwa bize.

Siku zikakatika. Kwa Fareed, maisha yalikuwa burudani lakini hakutaka kuendelea kuwa na mwanaume mmoja tu. Alitaka kila mwanaume mwenye mwili mzuri awe wake. Hakuacha kujiremba, alijipamba, alijua kujisafisha na kila alipokuwa, alikuwa akinukia maradhi ya Zenji, alijua kurembua macho, alijua kubinua midomo na zaidi ya yote alijua sana kuzungumza hasa kwa sauti ile ya kike.

Kwa wakati huo, alikuwa akijiandaa kwa safari ya kwenda Dubai. Alikuwa akimsindikiza mpenzi wake huyo aliyekuwa akienda kwa mambo ya kibiashara. Alichukua ndege pamoja naye, alivalia mavazi ambayo ilikuwa ni vigumu kugundua kama alikuwa mwanaume, alijiremba, alivalia dela na kichwani alivalia kiremba.

“Unakwenda Dubai?” aliuliza wakala wake aliyeitwa Asteria Kimaro, mwanamke aliyekuwa akiwaunganisha wanawake na wanaume tata kwa wanaume wengi waliokuwa wakiishi Ulaya, Asia na Marekani. Alijenga nyumba nyingi, kununua magari ya kifahari kwa biashara hiyo tu.

“Ndiyo!”
“Kuna wateja wawili wanakuhitaji huko. Nishafanya mawasiliano nao, nakutumia namba zao. Wanakuhitaji sana,” alisema Bi Asteria.

“Haina shida! Ila wana hela?” aliuliza Fareed, yeye alikuwa akifikiria hela tu.

“Eeh! Mtu aishi Dubai, awe mfanyabiashara mkubwa halafu asiwe na pesa! Umeona wapi hiyo! Hao wana hela mpaka wanaumwa!” alisema Bi Asteria.
“Basi sawa. Naomba namba zao!”

Akatumiwa namba hizo. Mwili wake ulikuwa ukiwasha mno, kila alipokaa, akili yake ilikuwa ikifikiria pesa tu. Hakutaka kuona akiishi maisha ya kimasikini, alijitoa maishani mwake, hapokuwa alikuwa akifanya jambo gumu, lenye kujidharirisha lakini hakuwa na jinsi, hayo yalikuwa maisha ambayo aliyachagua na alipaswa kuishi katika maisha hayohayo.

Walipofika Dubai, wakateremka ndani ya ndege, haikuwa mara yake ya kwanza, alikwishawahi kufika mara kadhaa hapo, wakatoka nje na kuchukua gari kisha kuelekea hotelini. Walipofika huko, ilikuwa ni kujiachia tu, walikuwa wakiyafurahia maisha, Godfrey alisahau kama alikuwa na mke, kwake, mwanaume huyo tata alimridhisha mno.

Usiku wa siku hiyo wakati Godfrey akiwa amelala huku amejichokea zake, Fareed akachukua simu yake na kuanza kupiga namba za wanaume aliokuwa amepewa. Alianza na mwanaume wa kwanza, huyu aliitwa Saed Al Muntazir, alikuwa mwanaume mwenye mwili uliojazia, ndevu nyingi, alikuwa mwanaume wa shoka, mweye pesa zake, kama alivyokuwa Godfrey, hata naye tabia yake ilikuwa ileile, kulala na wanaume tata kuliko hata wanawake.

“Nilipewa namba yako!” alisema Fareed, alikuwa amekimbilia chooni kuzungumza na mzee huyo.

“Kutoka wapi?”
“Kwa Asteria…”
“Ooh! Kumbe nini wewe! Hebu nitumie picha zako za utupu zikionyesha ulivyoumbika,” alisema mwanaume huyo.

Hiyo ilikuwa kazi ndogo kwa Fareed, hakutaka kuchelewa, hapohapo akamtumia picha hizo alizokuwa amekaa mikao ya hasarahasara, mwanaume huyo akazipokea, akaanza kuziangalia, mwili wake ukasisimka, hakuamini kama angekutana na mtu mwenye sura nzuri, umbo mashallaah kama alivyokuwa Fareed.

“Njoo hotelini kwangu!”

“Sawa. Nitakuja kesho asubuhi!” alisema Fareed.

“Sawa mpenzi!”

Hakutaka kukaa chooni kwa muda mrefu, akatoka na kurudi chumbani. Alipofika, macho yake yakatua kwa mpenzi wake, Godfrey ambaye alikuwa amekaa kitandani huku akionekana kuwa na hasira kupita kawaida.

Alivimba, alikuwa akipumua kwa hasira, paji lake la uso lilikunja ndita, kwa jinsi alivyoonekana, hakuonekana kuwa kwenye hali ya kawaida. Fareed aligundua kwamba kulikuwa na kitu, akagundua kwamba inawezekana mwanaume huyo aliyasikia mazungumzo yake alivyokuwa chooni, akaogopa kwani kuachwa na mwanaume huyo kulimaanisha angepoteza vitu vingi, starehe zote zingepaa.

Akaanza kumsogelea, hakuzungumza kitu, kwa mbali alionekana kutetemeka lakini hakutaka kulionyesha hilo, hakutaka agundulike kama alikuwa na hofu kubwa. Alipomfikia pale kitandani, akakaa pembeni yake na kuupitisha mkono wake katika bega la Godfrey.

“Tatizo nini mpenzi?” alimuuliza Godfrey.

Leave A Reply