The House of Favourite Newspapers

MIILI YA WATUMISHI WATANO WALIOFARIKI AJALINI YAAGWA DODOMA

MIILI ya watumishi 5 wa Wizara ya Kilimo na Chakula waliofariki katika ajali ya gari iliyotokea juzi Oktoba 21, 2018  eneo la Njirii wilayani Manyoni, Singida inaagwa leo katika Viwanja vya Wizara hiyo jijini Dodoma na baadae kusafirishwa kuelekea Bukoba na Dar es Salam kwa ajili ya mazishi.

Ajali hiyo ilihusisha magari mawili, moja lenye namba za usajili STK 8925 mali ya Wizara ya Kilimo na Chakula ambalo lilikuwa likitokea Dodoma kwenda Shinyanga, na lori (semi-trailer) lililokuwa likielekea Dar es Salaam lenye usajili wa RIC 152Y ambayo yaligongana uso kwa uso.

 

Watumishi waliofariki katika ajali hiyo ni;

1. Stella Ossano (39)

2. Esta Mutatembwa (36)

3. Abdallah Mushumbusi (53)

4. Charles Somi

5. Erasto Mhina (43).

BREAKING: Ajali mbaya ilivyoua 5 leo Singida

Comments are closed.