The House of Favourite Newspapers

Miji 10 Yenye Gharama Kubwa Zaidi Kuishi Duniani

 

PARIS ndio mji ulio na gharama kubwa zaidi duniani kimaisha, ukifuatiwa na Hong Kong na Singapore.

 

Ni mara ya kwanza miji mitatu imekuwa katika nafasi za juu katika historia ya miaka 30 ya utafiti wa kila mwaka wa uchumi – Economist Intelligence Unit —  unaolinganisha gharama katika miji 133 duniani.

 

Mji mkuu huo wa Ufaransa – uliokuwa katika nafasi ya pili kwa gharama kubwa ya maisha mwaka jana – ndiyo nchi pekee ya  Ulaya uliopo katika nafasi ya juu mwaka huu.

 

Utafiti huo umelinganisha bei za bidhaa za kawaida kama mkate katika miji 133.

 

Halafu inafuatilia iwapo bei hizo zimepanda au zimeshuka kwa kuzilinganisha na gharama ya maisha katika mji wa New York, Marekani.

 

Mhariri wa ripoti hiyo, Roxana Slavcheva, amesema Paris umekuwa mojawapo ya miji kumi iliyo na gharama kubwa zaidi kuishi tangu 2003.

 

“Ni pombe tu, usafiri na tumbaku ndiyo ulio na gharama nafuu ikilinganihswa na mataifa mengine ya Ulaya,” amesema.

 

Kiwango cha gharama kwa mwanamke kukatwa nywele, kwa mfano, hugharimu Dola za Marekani 119.04 mjini Paris, Dola 73.97 mjini Zurich na Dola 53.46 mjini Osaka nchini Japan.

 

Hii ndiyo miji 10 yenye gharama zaidi za maisha duniani

 

  1. Singapore (Singapore)

 

    1.Paris (Ufaransa)

 

1.Hong Kong (China)

 

4.Zurich (Uswizi)

 

5.Geneva (Uswizi)

 

5.Osaka (Japan)

 

7.Seoul (Korea ya Kusini)

 

7.Copenhagen (Denmark)

 

7.New York (Marekani)

 

10.Tel Aviv (Israeli)

10.Los Angeles (Marekani)

Comments are closed.