The House of Favourite Newspapers

Mikakati Mipya ya Tambwe ni hatari

 

WAKATI kikosi cha Yanga, juzi Jumatano kikifanikiwa kuibuka na ushindi dhidi ya Mbao FC katika mchezo wa Ligi Kuu Bara, sasa mambo ni moto kwa mshambuliaji wa timu hiyo, Mrundi, Amissi Tambwe.

Tambwe amekuja na mikakati kabambe ya kuhakikisha anaisaidia Yanga kufanya vizuri katika mechi zake zote zilizobakia huku akiwania tuzo ya mfungaji bora kimyakimya.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa baada ya kuifungia Yanga moja kati ya mabao yake mawili iliyoshinda dhidi ya Mbao FC, juzi Jumatano, alisema kuwa sasa njia hiyo ndiyo atakayotumia kuhakikisha anatimiza malengo yake hayo.

 

“Sina mengi ya kusema ila jambo kubwa nashukuru Mungu kwa kutuwezesha kupata matokeo mazuri dhidi ya Mbao ambayo ni moja kati ya timu ngumu zaidi inapokuwa kwenye uwanja wake wa nyumbani.

Comments are closed.