The House of Favourite Newspapers

SAKATA LA VITAMBULISHO VYA MACHINGA, SUGU AACHIWA

MBUNGE wa Jimbo la Mbeya Mjini ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’,  ameachiwa kwa dhamana na Jeshi la Polisi jana ambapo alishikiliwa tangu majira ya saa moja asubuhi  jana hiyohiyo,  Alhamisi Februari 21, 2019,  kwa tuhuma za kutoa/kutumia maneno ya uchochezi akiwa anazungumza na wafanyabiashara wadogo-wadogo.

 

Sugu anadaiwa kusema kwamba  vitambulisho vya wajasiriamali vimetolewa bila elimu na ni sawa na kunawa mikono kisha kwenda kujisaidia.

 

Kwa mujibu wa Mkuu wa Polisi Mkoa wa Mbeya (RPC)  Urich Matei,  ni kwamba Sugu ameonekana katika moja ya clip za video iliyosambaa katika mitandao ya kijamii akisikiliza hoja na malalamiko ya wananchi na kuyatolea ufafanuzi na ndipo alipoongea kwa kutoa msimamo wake kuhusu zoezi la ugawaji wa vitambulisho kwa wafanyabiashara wadogo-wadogo (wamachinga) na kusema havifai na vinastahili kuchomwa moto.

 

Matei amesema Sugu alisikika akitumia maneno ya kashfa dhidi ya mamlaka iliyotoa vitambulisho vya wafanyabiashara ndogondogo pia kutumia lugha zinazopinga zoezi la ugawaji vitambulisho kwa wafanyabiashara hao.

 

Sugu ametakiwa kuripoti tena leo asubuhi.

PASKO WA BSS alivyotembelewa na MAKONDA muhimbili

Comments are closed.