PENNY AJIPODOA KUFICHA SHIDA ZAKE

Penniel Mungilwa ‘Penny’

KUMBE! Kama ulikuwa hujui, basi chukua hii kutoka kwa mtangazaji wa Kipindi cha Harusi Yetu kinachorushwa kupitia Magic Swahili, Penniel Mungilwa ‘Penny’ ambaye amesanua kuwa kujipodoa huficha matatizo mengi.  

 

Mbele ya Gazeti la Ijumaa, Penny alisema mtu anaweza kukuona umependeza njiani na unanukia vizuri, akajua una mamilioni ya fedha kwenye pochi kumbe ni kujiweka vizuri tu ili kuficha shida zako.

 

“Mimi naweza kupita njiani mtu akadhani nina fedha nyingi maana napenda kujiweka nadhifu kila wakati ili tu heshima yangu ibaki palepale. Siyo hata mtu ukifulia kila mtu ajue, hapana haipendezi. Unaficha matatizo yako kwa kutokelezea chicha,” alisema Penny.

Na Imelda Mtema

Loading...

Toa comment