Mimba za Mastaa Hawa, Shehe Aanika Balaa Lao

Linah Sanga.

MASTAA wengi wamekuwa na tabia ya kupiga picha matumbo yao pale wanapokuwa wajawazito na kujianika mtandaoni wakidhani ni fasheni lakini imebainika kuwa wanaofanya hivyo wako hatarini kupatwa na mabalaa mazito, Risasi limeongea na Shehe mkuu wa Dar, alhad musa Salum.

 

Kiongozi huyo wa dini akizungumza na mwandishi wetu juu ya tabia hiyo iliyokithiri kwa mastaa wengi alisema, mbali ya kwamba dini zote zinakataza mwanamke kuanika sehemu nyeti za mwili wake, pia kuna madhara yanayoweza kuwapata wahusika.

Faiza Ally.

Alisema mastaa wanaofanya hivyo wanaweza kuhusudika kwani ni rahisi sana macho mabaya ya watu kuwadhuru wao wenyewe au watoto wanaokuwa tumboni. “Wanaopiga picha mimba tena tumbo wazi ni ushamba pia ni mambo yaliyo kinyume kabisa na dini zote, siyo kwenye Uislam tu bali kwa dini zote.

“Mwanamke anapokuwa na mimba anatakiwa kufanya siri mpaka atakapojifungua, wanaozianika mimba zao wanaweza kupata madhara makubwa au kiumbe kilicho tumboni kudhurika au ku
zaliwa na matatizo ya aina yoyote,” alisema shehe huyo.

Hamisa Mobeto.

Akaongeza kuwa, wengi ambao wanazaa watoto ambao hawajakamilika, wamekufa au wanazaliwa wakiwa na afya mgogoro, chanzo kinaweza kuwa ni jinsi mama zao walivyozilea mimba ikiwa ni pamoja na hilo la kuzianika mimba mitandaoni.

Msikie mama huyu Katika kuizungumzia tabia hii ya mastaa kujipiga picha wakiwa watupu kuonesha mimba zao, mama mmoja aliyejitambulisha kwa jina la mama Husna wa Sinza jijini Dar alisema: “Sisi enzi zetu haya mambo hayakuwepo kabisa, unakuwa mjamzito na mpaka unajifungua hakuna wa kuliona tumbo lako kirahisi zaidi ya mumeo.

Millen Magese.

Leo hii hawa mastaa wanatulelea utamaduni sijui wa wapi, na kweli inaweza kuwa ndiyo chanzo cha matatizo kwa watoto wengi wanaozaliwa. “Kubeba mimba ni heshima, sasa kuna ulazima gani kuitangaza kwa kulionesha litumbo lako na michirizi?

 

Ndiyo maana watoto wanazaliwa mataahira kwa sababu wameshapigwa ‘makombora’ tangu wakiwa tumboni kwa mama zao.” Mastaa waliowahi kupiga picha za mimba zao na kuanika mitandaoni ni pamoja na Zarinah Hassan ‘Zari’, Aunt Ezekiel, Hamisa Mobeto, Esterlina Sanga ‘Linah’, Millen Magesse, Faiza Ally na wengineo.

 

STORI: MWANDISHI WETU| RISASI| DAR ES SALAAM


Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment